Tuesday 22 January 2013

MAMBO SIO SHWARI KANISA LA MORAVIAN JIMBO LA MISHENI JIJINI DAR ES SALAAM

Kwa ufupi.
“Katika mikutano yake ya tume iliona njama za makusudi za kumpindua mwenyekiti kwa njia isiyo halali kwa sababu zisizojulikana, ukiukwaji wa maadili ya uongozi na Katiba ya Kanisa la Moravian (COUF) na katiba ya Jimbo la Mashariki,”
Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki Mch. Clement Fumbo akitangaza Halmashauri mpya ya kanisa hilo itakayokaa madarakadi hadi sinodi ya mwaka 2014.

HALI si shwari tena katika Kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki kutokana na Mwenyekiti aliyesimamishwa uongozi na Mkutano Mkuu wa Jimbo (Sidodi), Mchungaji Clement Fumbo kujichukulia madaraka na kutangaza uongozi wake mpya.

Fumbo alitangaza uongozi huo juzi katika ibada iliyofanyika katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Tabata akieleza kuwa uongozi wa juu wa kanisa unamtambua kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa kanisa katika jimbo hilo la Misheni.

Wakati hayo yakijiri sintofahamu imebakia kwa waumini kuwa hivi sasa waufuate uongozi upi wa mwenyekiti aliyesimamishwa na sinodi ama Makamu Mwenyekiti Sauli Kajura aliyepewa mamlaka ya kuliongoza jimbo hadi kipindi cha mkutano mkuu wa uchaguzi utakaofanyika mwaka 2014.

Kutangazwa kwa uongozi huo wa kanisa kumejiri wakati pia kesi ikiendelea katika Mahakama ya Kisutu ambapo Mchungaji Fumbo alifungua kesi ya kupinga uamuzi wa Sinodi akieleza kuwa hakuhusika na upotevu wa Sh 500m hali iliyosababisha avuliwe uongozi huo kupitia sinodi ya dharura.

Akielezea hisia zake kwa waumini wa Ushirika wa Tabata, Mchungaji Fumbo alisema ameamua kuunda uongozi mpya wa jimbo ili shughuli za kitendaji zisiweze kuendelea baada ya makamu mwenyekiti ,katibu na miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu kusababisha mpasuko kati ya waumini na wachungaji.

Mchungaji Fumbo alisema Juni 5, mwaka 2012 yalifanyika mapinduzi ya kumwondoa madarakani yeye  watendaji, na baadhi ya Wakristo kutengwa huku wachungaji wakitishiwa maisha kinyume na taratibu za kanisa hilo.

Alisema jambo hilo lilisababisha mgawanyiko ndani ya kanisa kwa ngazi ya viongozi na kuambukiza wachungaji na walei wa kanisa la jimbo hilo hata kwenye majimbo mengine ambayo yana masilahi na jimbo hilo.

Fumbo alisema Kanisa la Moravian Duniani (COUF)kupitia kwa mwakilishi wake umeingilia kati na kutuma ujumbe wake ambao ulikuwa Novemba 25,26, na 27 mwaka 2012 kwa lengo la kutafuta kiini cha mgogoro ili kupendekeza suluhisho lake.

“Katika mikutano yake ya tume iliona njama za makusudi za kumpindua mwenyekiti kwa njia isiyo halali kwa sababu zisizojulikana, ukiukwaji wa maadili ya uongozi na Katiba ya Kanisa la Moravian (COUF) na katiba ya Jimbo la Mashariki,”alisema na kuongeza:

“Kutokana na hayo tume imeagiza yawepo mazungumzo ya pande mbili yanayolenga kurudi kwenye mfumo wa uongozi wa mwaka 2010 na kufuata taratibu za mambo yaliyosababisha kukosa maelewano na uchunguzi wa kina ufanyike kubaini kiini cha tatizo,”alisema Fumbo.

Alisema msuluhishi wa Kanisa la Moravian Duniani (COUF) alinyimwa ushirikiano kutoka kundi la Makamu Mwenyekiti na Katibu wake ambapo hawakutaka kusuluhishwa ili mgogoro umalizike.

Alisema kwa kuwa kanisa linahusu imani za watu kwa kuzingatia kwamba uongozi uliochaguliwa mwaka 2010 ukiwa chini ya mwenyekiti Fumbo haujamaliza muda wake mwaka 2014 ambapo ukizingatia yalifanyika mapinduzi ya kuondoa baadhi wa viongozi wa jimbo hilo (HAIJAMALIZIKA).

No comments: