Friday, 7 June 2013

MADIWANI WA HALMASHAURI YA KYELA WAPITISHA PENDEKEZO LA KUGAWANYWA KWA MKOA WA MBEYA




Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya kyela wamepitisha pendekezo la mkoa Mbeya kugawanywa na mkoa mpya uitwe Rungwe na makao yake makuu yawe mjini tukuyu.
Katika mapendekezo yaliyo kaliwa na kamati ya fedha ,uongozi na mipango ilipendekeza hivyo kwa kufuata vigezo mbalimbali ikiwemo Jiografia ya maeneo ,historia ya wilaya husika ,shughuli za kijamii na kiuchumi sambamba na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Wilaya zilizo pendekezwa na baraza la madiwani kyela kuunda mkoa mpya wa Rungwe ni Kyela,Rungwe na halmashauri zake ikiwemo ya Busokelo na wilaya ya Ileje huku Mbeya ikibaki na Mbozi,Momba,Mbarali na Chunya.
Asilimia tisini na tisa ya madiwani wote wameunga mkono makao makuu yawepo Rungweingawa baadhi yao walitaka makao makuu yawe Busale wilayani Kyela kitu ambacho wengi wao hawakukubaliana nacho.{Na Israel Mwaisaka}

No comments: