Friday 14 June 2013

MOURINHO AISHIKA PABAYA MAN UNITED, SASA AAMUA KUMSAINI LEWANDOWSKI...TORRES, BA HAWANA CHAO TENA DARAJANI


IMEWEKWA JUNI 14, 2013 SAA 2:00 USIKU
KLABU ya Chelsea imehamishia mawindo yake kwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski katika harakati za kocha Jose Mourinho kusaka kiongozi wa safu ya ushambuliaji.
Mourinho hashawishiki na Fernando Torres na Demba Ba na wanataka mtu mwingine katika safu ya ushambuliaji kupambana na nyota kinda, Romelu Lukaku na mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 18, Andre Schurrle ambaye wazi atakuwa anacheza pembeni.
Lewandowski anataka kuachana na wana fainali hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, lakini Dortmund imegoma kumuuza kwa wababe wao, Bayern Munich, ambako alichagua.
PL bound? Lewandowski is expected to be on the move this summer after some fine seasons in Germany
Atatua England? Lewandowski anatarajiwa kuhama baada ya kufanya vizuri kwa misimu kadhaa Ujerumani
PL bound? Lewandowski is expected to be on the move this summer after a number of fine seasons in Germany
Unconvinced: Mourinho's does not see enough in his strikers to shoot them to the top
Hashawishiki: Mourinho haoni kama washambuliaji wake watatosha kuiweka timu kileleni

Mwakilishi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amewasiliana na Chelsea, Manchester United, Real Madrid na Barcelona pamoja na Bayern juu ya uhamisho wa Pauni Milioni 25.
Dortmund haiko tayari kumuuza kwa Bayern, baada ya mabingwa hao wa Ujerumani na Ulaya kuwachukulia mchezaji wao mwingine, Mario Gotze kwa dau la Pauni Milioni 32 mwezi uliopita.
Wiki iliyopita, Mtendaji Mkuu wa klabu, Hans-Joachim Watzke aliliambia Bild: "Robert Lewandowski hatauzwa kwa FC Bayern mwaka 2013. Hiyo ni mwisho. Tumemuambia Robert na wakala wake sasa,"alisema.
Striking options: Lewandowski could be seen as a cheaper option to Cavani (left) while Schurrle could play out wide
Striking options: Lewandowski could be seen as a cheaper option to Cavani (left) while Schurrle could play out wide
Suluhisho la ushambuliaji: Lewandowski anaweza kuwa suluhisho jepesi kwa Cavani (kushoto) wakati Schurrle atacheza pembeni.

Hiyo inaweza kufungua milango kwa Chelsea, ambao wanaendelea taratibu kuisaka saini ya thamani ya Pauni Milioni 54 ya mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani.
Cavani anatakiwa kwa muda mrefu Chelsea, lakini Mourinho ni shabiki mkubwa wa Lewandowski aliyemshuhudia akifunga mabao manne dhidi ya timu yake ya zamani, Real katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Chelsea bado pia inamfukuzia mshambuliaji wa Zenit St Petersburg, Hulk, lakini Manchester United haiko tayari kumruhusu Wayne Rooney ahamie Stamford Bridge.

No comments: