Asasi ya Pambana Saidia
Jamii[SCSA]wilayani kyela imetoa msaada wa shilingi milioni tano kwaajili ya
kutengenezea madawati mia moja katika shule ya msingi Ikombe.
Akikabidhi msaada
Mwenyekiti wa Asasa hiyo Edward Nkyandwale amesema,kwakushirikiana na Wananchi
wa Ikombe wameweza kutengeneza madawati hayo.
Hata hivyo Nkyandwale
amewaasa viongozi na wananchi wa Ikombe
kuacha siasa, badala yake waungane na
wafanye kazi pamoja ili waweze kuleta
maendeleo katika kijiji chao, pia amesema hawatokuwa tayari kusaidi wananchi pasipo wao
kuchangia chochote.
Akizungumza kwa niaba
ya Wananchi Mwenyekiti wa kijiji Method Kilongo, ameishukuru Asasi hiyo kwa
msaada waliotoa na kuomba wasichoke kusaidia pindi watakapohitaji msaada katika
miradi mingine.{Na Frank Mwakatundu Kyela}
No comments:
Post a Comment