Thursday, 6 June 2013
WANANCHI WA IKOMBE KYELA WA PINGA AGIZO LA SERIKALI
Wananchi wa kijiji cha Ikombe Kata ya Matema wilayani KYELAwamepinga agizo la serikali la kutokufanya shughuli zao za kilimo katika hifadhi ya milima ya Livingstone,ambalo lilitolewa na Ofisa Misitu na mazingira Aswile Fumbo katika mkutano uliofanyika katika kitongoji cha Lyulilo tarehe 28 May mwaka huu akimuwakilisha mkuu wa Wilaya Magreth Malenga.
Wananchi wameyasema hayo katika mkutano wa Diwani wao wa kata ya Matema Issah Solomon Mwatwebe uliofanyika tarehe 4 June mwaka huu katika kijiji cha Ikombe.
Aidha wamepinga agizo hilo kwa madai kwamba serikali haikuwatendea haki kwakufanya mkutano nakitongoji kimoja badala ya kwenda kufanya mkutano makao makuu ya kijiji ambapo wangeweza kukutana na wananchi wote wakijiji hicho.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kijiji Method Kilongo amewataka wananchi wawe wavumilivu wakati viongozi wao wanafanya utaratibu wa kuiomba serikali iweze kufika katika kijiji hicho kuzungumzia kero hiyo.{Na Franck Mwakatundu Kyela}
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment