Wednesday, 5 June 2013

WATOTO WAWILI WAUAWA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA MBALIZI


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athumani.

WINGU zito la mauaji ya watoto wawili katika eneo la Mageuzi kijiji cha Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya, limezidi kutanda ambapo watoto hao wanasadikika kuuawa na kaka yao kwa ushirikiano na mama yao ili waongeze utajiri.

Habari zinasema kuwa kutokana na tukio hilo lililotokea Mei 29, mwaka huu. 

Mama mzazi wa watoto hao ameamua kufunguka na kuwaomba radhi majirani kuwa wasishikane uchawi maana kitendo hicho alikifanya mwanaye mkubwa ambaye ni mfanyabiashara wa eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Watoto waliokutwa wamekufa katika mazingira tata ni Daud na Baraka.

No comments: