Katika
hali inayoonyesha TAMISEMI kugusa maeneo oevu ya baadhi ya mabaraza ya
madiwani nchini, hatua yake ya kutoa waraka wa shughuli za ukaguzi wa
miradi kufanywa na kamati ya Fedha,Utawala na Mipango FMU imeonekana
kuwa mwiba mchungu kwenye baraza la halmashauri ya Mbozi baada ya
waheshimiwa madiwani kutaka kuazimia kinyume cha kanuni maelekezo kutoka
ngazi za juu! story kamili inafuata----
kutoka
kushoto ni Makamu mwenyekiti ALAN MGULA, akifuatiwa na Mwenyekiti
ERICK AMBAKISYE na akifuatiwa na DED MBOZI Levison Chilewa
michango ilianza hivi
Hawa watunga sheria wa baraza la Mbozi wakiwa hewani kama hivyo wakati kikao kikiendelea
Mh
Emily Mzumbwe akichambua suala la uchangiaji wa hisa kwenye benki ya
wananchi wa Mbozi ambapo limeonekana kurudisha reverse na madiwani baada
ya kutaka mchakato huo usipelekwe puta kwa maelezo kuwa lazima wananchi
waelimishwe pole pole namna ya kuchangia hisa zao badala ya kukata juu
kwa juu sehemu ya fedha kwenye mauzo ya kahawa yao
Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya MBOZI wakisikiliza majadiliano
Kulia
wa kwanza ni katibu tawala Mbozi bwana Lazaro Mwankenja akifuatiwa na
Mkurugenzi Mtendaji Mbozi bwana Levison Chilewa wakifuatilia upepo
unavyokwenda kwenye baraza hilo
AFISA
utumishi Bwana Zabron Lulandala akifuatiwa na afisa Mipango wilaya
bwana Ngoi wakifuatilia mijadala kwenye baraza la madiwani leo
Baadhi
ya watendaji kutoka ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi pamoja na
ofisi ya mkuu wa wilaya wakifuatilia mijadala kwenye baraza hilo leo
Hali
hiyo ilijitokeza baada ya madiwani kupitia kamati zao kuanza kulalamika
hatua iliyofikiwa ya kuzuiwa kwenda kukagua miradi wakiwa kwenye kamati
zao na badala yake kupewa maelezo kuwa kuna waraka unaozuia kamati hizo
kutokana na kukosekana ufanisi!
Ndipo
miongozo mwenyekiti, azimio na maneno mengine ilipoanza kusikika,
lakini mwishowe ikawa ngumu kurudisha wwaraka huo TAMISEMI na badala
yake madiwani kukubaliana nao kwa shingo upande
Hatua
hiyo ilifikiwa\ baada ya ufafanuzi kutolewa kuwa kimsingi serikali za
mitaa pamoja na kuwa ni muhimili muhimu katika kuunganisha wananchi na
kuleta maendeleo haimaanishi kuwa serikali kuu haina nguvu ya kuelekeza
jambo mbele ya serikali za mitaa.
Na
kwamba kwa kutambua hilo ndiyo sababu halmashauri kwa sehemu kubwa kama
siyo asilimia 95% hutegemea ruzuku kutoka serikali kuu, hivyo pale
inapoagizwa baadhi ya mabadiliko ngazi za chini hakuna lugha ya
kuyapamba maelekezo hayo bali kuyatekeleza
Ndipo
diwani mmoja akasimama na kuomba mwongozo kisha akachomekea na azimio!
hata hivyo mwenyekiti wa baraza hilo akatoa ufafanuzi kuwa serikali
haiwezi kuazimiwa kwakuwa baraza hilo limeundwa pia kutokana na
maelekezo na miongozo kutoka juu hivyo waheshimiwa wawe wapole kwanza!
katika
hatua nyingine suala la uanzishwaji wa benki ya wananchi ya Mbozi leo
limeendelea kupigwa dana dana ya kukubaliana kuto kubaliana! baada ya
madiwani kuunga mkono kuanzishwa kwa benki hilo lakini wakitaka wananchi
waleweshwe pole pole na pia wapate ziara ya kwenda kujifunza mikoa
mingine namna ya benki hizo zinavyofanya kazi
Katika
hali inayoonyesha kuwa wimbi hilo lilishawekwa mapema, kila
aliyenyanyuka alikuwa akiongezea misumali ya kuzuia kuharakishwa
kuchangisha shilingi 200 kwa kilo ya kahawa kwaajili ya uanzishaji wa
benki hiyo ambapo baada ya maelezo ya ufafanuzi ya mkurugenzi mtendaji
wilaya ya MBOZI, bado suala hilo liliamuliwa kwa kutakiwa kwanza wapewe
ziara na baadaye wananchi waelimishwe namna bora ya kushiriki uanzishaji
wa benki hiyo.
No comments:
Post a Comment