Wednesday 24 June 2015

Kipindupindu Chalipuka tena Kigoma


WATU watatu wamefariki dunia katika Kijiji cha Kalagu  kwenye mwambao mwa Ziwa Tanganyika Wilaya ya Kigoma Vijijini   kutokana na  mlipuko wa   kipindupindi  huku wengine 10  wakiwa wamelazwa katika zahanati ya Gungu.
 
Akizungumza na chanzo cha habari Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Leonard Subi,  alisema mpaka jana kulikuwa na wagonjwa 10 waliolazwa katika  Zahanati ya Mwakizega ya wilayani Uvinza  na watatu wamefariki dunia.
 
Dk. Subi alisema ugonjwa huo umelipuka kwa wananchi wanaoishi mwambao wa Ziwa Tanganyika kutokana na  kuwapo  raia wa kigeni  kutoka  nchi ya jirani ya Burundi  ambao wanakuja nao.
 
Aliwaomba wananchi kuchukua tahadhari kutokana na ugonjwa huo kwa kuchemsha maji ya kunywa, kunawa mikono   na kula chakula cha moto.
 
Idara ya  afya ya mkoa wamejipanga kuweka mikakati ya kupambana na ugonjwa huo na kuhakikisha maji yote yanawekewa dawa kabla hayajafika kwa watumiaji, alisema.
 
"Ninawaomba wananchi waendelee kuchukua tahadhali kutokana na mlipuko huu wa   kipindupindu ambao ni hatari…  naomba  wananchi wahakikishe wanaweka mazingira katika hali ya usafi na waache tabia ya  kula kula hivyo,” alisema  Dk. Subi.

No comments: