Thursday, 14 March 2013

TGNP yashinda kesi ya Jengo Mahakama Kuu

 Jengo lenyewe la TGNP
Usu Mallya

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), walinunua  jengo la ofisi hii kutoka kwa Mfilisi wa iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited (TSTML) yaani Benki ya Rasilimali ya Tanzania mnamo tarehe 15th June, 1997. 

Wapangaji wasiohalali walikwenda mahakamani wakiwashitaki Benki ya Rasilimali ya Tanzania pamoja na TGNP na kesi ilifunguliwa tarehe 16th July 1997 kesi ilipewa Na. 215/1997. Madai ya washitaki yalikuwa yafutayo:
    a)        TGNP ilipendelewa katika mchakato mzima wa tenda ya manunuzi ya jengo hili na kwamba TGNP hawakuwa wazawa.
   b)        Utoaji wa tenda kwa upande wa Beki ya Rasilimali Tanzania ulikuwa batili kwa sababu haukufuata/haukuzingatia sheria ya nchi ya manunuzi na hivyo kukiuka haki za kimsimgi (failure to observe the law, public policy and the rules of natural justices)

TGNP kama washitakiwa walishinda kesi hiyo ya  madai namba 215/1997 iliyofunguliwa na waliokuwa wapangaji. Jengo lenye kesi ni jengo la gorofa moja zilipo Ofisi za Makao Makuu ya Shirika Mabibo Dar es salaam.

Chini ya Mhe. Jaji T.B. Mihayo, 15 Oktoba 2009, TGNP Ilishinda kesi hiyo na walalamikaji walidai kuwa TGNP imependelewa. Oktoba 19, 2009, walifungua rufaa katika makahakama kuu ya Rufaa ya Tanzania, wakiipinga hukumu ya kesi ya msngi namba 215/1997 na kukawa na kesi ya rufaa namba 129/2009 ili pia waendelee kukaa kwenye jesngo hilo.

TGNP iliiomba mahakama kufuta ombi la walalamikaji la kuendelea kuwa kwenye jengo ili shirika liweze kufanya shughuli zake, kesi ambayo ilisikilizwa na majaji watatu waheshimiwa jaji Msasali, jaji Msofe, na jaji Rutakanga Julai 22,2011.

Tarehe 23. 08.2011, TGNP iliamua kwa mujibu wa sheria kuwatoa kwa nguvu wapangaji hao ambao kwa muda wote wa zaidi ya miaka 10 wamekuwa wakifanya shughuli zao kwenye jengo la TGNP bila kulipa kodi wala ruhusa yao, lakini siku chache baadaye walirudi. Pamoja na ushindi walioupta TGNP bado waliendelea kuheshimu maamuzi ya mahakama kutokana na shauri walilolipeleka mahakamani.

Mwaka 2012 walalamikaji walienda tena Mahakama Kuu wakiomba kurekebisha majina ya watu waliosomewa hukumu kuwa  watu wengine walio hukumiwa hawakuwa sehemu ya kesi hii!!  TGNP tuliona kuwa hii ni  mbinu tuu ya kuchelewesha  kesi ambayo imekuwa ikitumika  kwa miaka mingi. Jaji Mwaikugile aliikubali hiyo barua akitaka wakaandike vizuri zaidi ili hoja yao isikilizwe. Kesi hii imepangiwa kusikilizwa tena hapo tarehe 26 Februari 2013, lakini hadi tarehe 08.03.2013 hawakuwa wamewasilisha na leo tarehe 13.03.2013 jaji ametupilia mbali ombi lao.

Kesi hii imekuwa ni changamoto kwa TGNP, huu ni mwaka wa 16 tangu shirika linunue jengo hili.

Sote kwa pamoja tunaamini katika haki na na rasilimali lazima zirudi kwa wananachi!

Imetolewa na:
Usu Mallya
Mkurugenzi Mtendaji TGNP

No comments: