RAIS Dkt. Jakaya Kikwete, ametamba kuwa angakuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya basi angelikuwa wa “BongoFleva” kutokana na kuwa na sauti nzuri yenye kumudu kuimba nyimbo kwa ufasaha zaidi.
Kauli hiyo aliitoa jana jijini Mwanza kwenye uwanja wa michezo wa CCM Kirumba wakati wa maadhimisho ya kilele cha sherehe za Mei mosi zilizofanyika Kitaifa jijini Mwanza kwa mwaka huu wa mwisho wa utawala wake.
Dkt. Kikwete aliimba wimbo wa Bendi ya OSS (Ochestra Safari Sound) wenye mashairi yasemayo "Mimi msafiri bado niko njiani sijui lini nitafika... naulizia watu kule ninakokwenda....” na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliomshangilia ambapo alijiamba kuwa na sauti ya mauzo.
“Mmesikia sauti yangu si mbaya sana, hakika nisingekuwa Rais wa Nchi hii basi nigekuwa msanii wa bongo fleva kama akina Ali Kiba, Diamond na wasanii wengine wakali nikiuza album zangu kwani ningekuwa tishio kwa kuimba...” alisema.
Rais pia alimpongeza msanii maarufu nchini wa kizazi kipya mwenye mashairi na misamiati ya maneno magumu, Mrisho Mpoto, kwa kumtaka kujibu bango la walimu lililokuwa na ujumbe uliosomeka “Shemeji Unatuachaje??” ambapo alijibu kwa kusema kuwa "kuoa mwalimu nitabu kweli kweli haya nimesikia."
Aliwapongeza viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) nchini kwa kumwalika Mpoto “Mjomba” .Mara nyingi amekuwa akitoa ujumbe mzito kupitia fani yake ya muziki na mashairi lakini yakifikisha ujumbe bara bara kwa wananchi katika sherehe mbalimbali za kitaifa na makongamano .
No comments:
Post a Comment