Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Siro ameagiza wafanyabiashara na
watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi nchini kuchukuliwa hatua kali
kwani wanarudisha nyuma na kuchelewesha maendeleo ya nchi.
IGP
Sirro amesema hayo jana alipofanya ziara mkoani Mbeya na kuwaagiza
askari wa vikosi mbalimbali vya polisi kuhakikisha wanawakamata na
kuwachukulia hatua za kisheria watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi.
"Kuna
watu wanafikiri ni sifa kufanya magendo wote tunajua umuhimu wa kulipa
kodi kwa hiyo tumepanga mpango mkakati wa kuwashughulikia vizuri sana
wale ambao wanakwepa kulipa kodi, wananchi wetu wanapaswa kubadilisha
mtazamo wao waone wanawajibika kwenye kulipa kodi sababu kodi ndiyo
inafanya maendeleo ya nchi yetu, kodi ndiyo inaleta madawa, kodi inaleta
barabara na kodi ndiyo kila kitu. Na wale ambao wanakwepa kulipa kodi
nimetoa maelekezo kuwashughulikia kila mahali na kila siku wanasikia
Amiri Jeshi Mkuu anazungumzia habari hii sasa wewe unayekwepa kulipa
kodi ni nani" alisisitiza Sirro
Aisha
IGP Sirro aliwataka wafanyabiashara pamoja na wananchi kulipa kodi ili
nchi iweze kupata maendeleo na kusonga mbele zaidi.
No comments:
Post a Comment