Wakili
wa kujitegemea, Peter Kibatala ameandika waraka kwa Rais wa chama cha
Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ,Tundu Lissu kwamba atahakikisha
anatumia ujuzi wake wote wa sheria kuhakikisha katazo la IGP Sirro
kuhusu mjadala wa kiongozi huyo kupigwa risasi linatenguliwa.
Kibatala
ameweka waraka wake kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa yamepita
masaa machache baada ya IGP Sirro kutoa kauli ya katazo kwa wanasiasa
kuhusu kuuendeleza mjadala wa Lissu na kuwataka waliachie jeshi la
polisi liendelee kufanya kazi yake.
Kibatala
ameandika "Mpendwa Kaka Tundu Lissu wanasema eti wamekataza mjadala juu
ya wewe kupigwa risasi 11 mwilini mwako, kati ya zile 38 zilizoelekezwa
kwako.binafsi nitatumia ujuzi wangu wote wa kisheria kuhakikisha hilo
katazo linatenguliwa. Ile tu kupambana kuhakikisha hicho kitu hakina
mashiko kisheria ni sehemu ya kutimiza wajibu wangu kwako .
Waraka
ukaelezea zaidi; "U are my President, now and forever, my whole some
President na i will be very stupid to leave such legal issues
un-attended". (Nitakuwa mpumbavu nikiiacha ishu hii ya kisheria bila
kuishughulikia Rais wangu, Wewe ni rais wangu sana na hata milele".
Hata
hivyo katika waraka wake huo Kibatala ameomba radhi kwa Rais wake huyo
kwa kutowekeza nguvu zake kwenye sintofahamu za Msaidizi wa Mwenyekiti
wa Chadema Taifa Ben Saanane aliyepotea kusikojulikana na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Alphonce Mawazo aliyeuawa na watu
wasiojulikana, huku akimuahidi kuanza kutafuta ufumbuzi wa kisheria
kwenye masuala hayo.
"Nisamehe
sikuwekeza nguvu za kisheria za kutosha kwenye issues za Ben Saanane na
Alphonce Mawazo. Mimi na wenzangu tutatumia kila mbinu ya kisheria
kuhakikisha mambo haya yanapatiwa ufumbuzi wa umma kwa sababu upelelezi
kisheria si mali binafsi ya jeshi lolote nchini" Kibatala ameongeza.
Kibatala
ameongeza "Tundu Lissu ukirudi utanikuta nipo njiani na masuala haya na
kwa vyovyote wewe au mwingine 'who will be left standing or sitting,
will carry through' .
Hata
hivyo mwisho wa waraka huo Kibatala amesema ajenda yake kuu wiki hii
itakuwa pia ni kuuliza kisheria uhalali wa kuzuia maombi ya wazi kwako
Tundu Lissu.
No comments:
Post a Comment