WAANDISHI IRINGA WAZINDUA IPC VIKOBA KWA KISHINDO WAPATA TSH M. 7.4
MLEZI
wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) na mfanyabiashara
maarufu wa mjini Iringa, Salim Abri (Asas) achangisha kiasi cha zaidi ya
shilingi milioni 7.4 huku mwenyewe akiwachangia wanahabari Iringa kiasi
cha Milioni 2 taslimu katika harambee ya kuchangia asasi ya kuweka na
kukopa ya wanahabari wa mkoa wa Iringa (IPC Vicoba).
.
Katika
harambee hiyo iliyofanyika jana kwenye Mkutano Mkuu wa Wadau wa Habari
uliofanyika katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa blog ya Francis
Godwin iliahidi kuchangia kiasi cha shilingi 200,000 Blog ya Mjengwa
aliahidi 100,000 wakati mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi akichangia
shilingi 300,000 pamoja na benki ya wananchi Mufindi ambayo pia iliahidi
kuchangia kiasi cha shilingi 300,000.
Wengine
waliochanga katika harambeee hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Iringa Jesca Msambatavangu Sh 200,000, Mkuu wa Wilaya Kilolo, Gerald
Guninita Sh 200,000 ,na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM) Rita
Kabati (CCM) Sh 100,000.
Jeshi
la Polisi waliahidi kuchangia Sh 300,000, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk
Christine Ishengoma Sh 100,000 Mkurugenzi wa kampuni ya Ujenzi ya GNMS
Geofrey Mungai Sh 150,000 na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dk Leticia Warioba
Sh 100,000.
Aidha baraza la vijana la Chadema (BAVICHA) liliahidi shilingi 100,000,UVCCM Iringa vijijini 100,000,Mwakilishi wa Habari leo Iringa (100,000),IMTV(100,000)Country Fm (100,000),Nuru Fm ( 70,000), Ebony Fm (80,000),Qbla Ten (50,000), Furaha Fm(50,000),ICISO (100,000) madiwani Manispaa ya Iringa (250,000) na wengine wengi.
Wengine
akiwemo Mhifadhi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa), vyombo
vya habari vya mkoani na wadau mbalimbali walichanga kati ya Sh 50,000
na Sh 100,000 huku wanahabari wenyewe wakichanga zaidi ya Sh Milioni 2.
Akishukuru
kwa michango hiyo, Mwenyekiti wa IPC Vicoba Janeth Matondo aliwashukuru
wadau wa habari mkoani hapa kwa kukisaidia chama hicho kupata mtaji.
“Mtaji huu utatumika kuboresha shughuli mbalimbali za kimaendeleo za wanahabari mkoani hapa,” alisema.
Alisema
pamoja na kukopeshwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufanyia kazi,
mikopo mingine itakayotolewa italenga kuinua shughuli za kijasiriamali
za wanahabari wa mkoa wa Iringa.
Awali
Salim Abri ambaye pia ni mlezi wa Klabu ya Wanahabari Mkoa wa Iringa
(IPC) aliwapongeza wanahabari kwa kuanzisha chama hicho.
“Ndugu
zangu wadau, wanahabari ni watu muhimu sana katika kusukuma gurudumu la
maendeleo ya taifa, lakini wengi wao hawajaajiriwa, wanafanya kazi kwa
malipo haba, kwahiyo chombo hiki kitasaidia kubadili maisha yao,”
alisema na kuwasihi wadau walioahidi kutoa michango kutimiza ahadi zao.
Aliutaka
uongozi wa IPC kufuatilia michango iliyoahidiwa na kuomba michango
zaidi kutoka kwa wadau wengine ili kukiimarisha chombo hicho.
Wakati katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard alisema kuwa lengo la kuanzisha IPC VIKOBA ni kutaka wanahabari mkoa wa Iringa kujitegemea na kutumia chombo hicho kukopa kwa ajili ya kujenga nyumba ama kununua vitendea kazi .
No comments:
Post a Comment