SAKATA
la uchinjaji kati ya Waislamu na Wakristo limeingia katika sura mpya baada ya
waumini wa madhehebu hayo katika Mji wa Tunduma wilaya ya Momba mkoani Mbeya,
leo kuamua kujichinjia wenyewe katika machinjio moja ya serikali.
Kwa
mujibu wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo
wameeleza kuwa asubuhi ya siku ya Pasaka Machi 31, zilichinjwa jumla ya ng’ombe
40 ambapo inadaiwa kuwa kati ya hizo ng’ombe 3 walikuwa wa waislamu na 37
walikuwa wa wakristo.
Silanda
Barton ni mmoja wa mashuhuda hao alisema kuwa, baada ya uchinjaji huo kufanyika
alifika mkaguzi wa nyama ambapo alishitushwa na hali ambayo haikuwa ya kawaida
ndipo alipokagua nyama ya ng’ombe watatu waliochinjwa na waislamu na kuamua
kuacha hali ambayo iliwafanya wengine kuamua kuzuia nyama hiyo isiuzwe.
Barton
alisema hata hivyo wateja waliofika buchani siku ya leo ili kujipatia kitoweo
hicho walifanya jitihada za kumuomba afisa mifugo huyo ili aweze kukubali
kupima nyama nao wajipatie kitoweo.
Hata
hivyo Afisa Mifugo huyo ambaye ametambulika kwa jina moja la Tarimo alikubali
kufanya ukaguzi na ndipo nyama ikaanza kuuzwa mchana.
Alisema
Wakati mzozo huo ukiendelea kundi moja
la vijana (Vibaka) waliingilia kati kwa lengo la kuukuza ili patokee vurugu
ambazo zingewanufaisha kwa kupora mali.
Aidha
kutokana na hali kutokuwa washari jeshi la polisi kikosi cha kuzuia ghasia
(FFU) kilifika katika eneo hilo
ili kuimarisha ulinzi zaidi.
Mkuu
wa wilaya ya Momba Abihudi Saideya alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi
hakuweza kupokea na alipopigiwa dereva wake alidai yupo katika eneo la tukio
kujaribu kuweka mambo sawa.
Vurugu
katika mji wa Tunduma zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara ambapo lipo kundi la
vijana ambalo limekuwa likishabikia mambo ili kuyakuza kwa lengo la iwapo itatokea
vurugu lipata nafasi ya kupora mali.
No comments:
Post a Comment