Wednesday, 29 April 2015

Waziri Magufuli aushukia uongozi unaojenga barabara ya mabasi yaendayo kasi DART jijini Dar es Salaam.


Waziri wa ujenzi Dokta John  Magufuli ameuagiza uongozi wa kampuni inayojenga barabara za mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam  kufanya kazi usiku na Mchana katika kuhakikisha ujenzi wa barabara hizo unakamilika kwa muda uliopangwa ili kuondokana na kero ya msongamano wa Magari.
Doka magufuli ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua mradi wa barabara za mwendo wa haraka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambapo barabara hizo zinajengwa pamoja na kuweka jiwe la msingi barabara na upanuzi wa barabara kwa njia nne kwa barabara ya  Uhuru hadi Buguruni malapa na kusema miradi yote hadi kukamilika kwake utagharibu shilingi trilioni 1.52 ikiwemo mradi wa DARTS.
 
Kadhalika Mh. Magufuli katika mpango wa ujenzi wa barabara za pembezoni mwa mji ikiwemo eneo la mbagala tayari serikali ina mpango wa kujenga sita za chini na juu kutoka mbagala charambe hadi chalinze mradi unaotarajiwa kuanza kutekelezwa muda wowote kuanzia sasa lengo likikiwa kumaliza foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam huku mtendaji mkuu wa wakala wa barabara nchi TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale amesema mradi wa DARTS ambao utakuwa wa awamu sita kwa sasa umefikia hatua ya majaribio ya awali kabla kukamilika kwake.

No comments: