Watu kumi na tano wamejeruhiwa na wengine zaidi ya hamsini wakinusurika kufa baada ya basi la kampuni ya TAKBIR Lililokuwa likitokea mkoani geita kuligonga basi la kampuni ya ABOOD,maeneo ya Lubungo Mikese katika barabàra kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.
Ajali hiyo imehusisha basi aina ya SCANIA,mali ya kampuni ya TAKBIR lenye namba za usajili T.230 BRG,lililokuwa likitokea mkoani Geita, kuelekea jijini Dar es Salaam, likiendeshwa na PROJETUS MODESTUS, mkazi wa mabatini mwanza ambalo kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo,limeligonga kwa nyuma basi la kampuni ya ABOOD lililokua likitokea Morogoro kuelekea Dar es Salam likiendeswa na Abdala Hemed, mkazi wa kiwanja cha ndege Morogoro na kusababisha idadi hiyo ya majeruhi,wakiwemo wanawake wanane, wanaume watano pamoja na watoto wawili,huku dereva wa TAKBIR akidaiwa kukimbia baada ya ajali.
Nao majeruhi wa ajali hiyo wamebainisha chanzo cha ajali ni dereva wa basi hilo kutokua makini na kuendesha gari kwa mwendokasi,na kwamba wanashukuru wanaendelea na matibabu, huku kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Leonard Paulo akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kutambua kuwa wanabeba roho za wananchi na hatma ya roho hizo iko mikononi mwao.
No comments:
Post a Comment