Tuesday, 30 October 2012

Mshahiri maarufu auawa nchini Somalia


 
Awale alikuwa anapinga sana kauli mbiu ya harakati za Al Shabaab na huenda aliuawa kwa ajili ya hilo
Watu wasiojulikana na ambao walikuwa wamejihami kwa bunduki nchini Somalia, wamemuua mshairi, muimbaji na mtumbuizaji maarufu, Warsame Shire Awale. Kwa mujibu wa muungano wa kitaifa wa waandishi nchini Somalia.
Awale amekuwa akipokea vitisho hivi karibuni vinavyohusika na matamshi aliyotoa kuhusu watu waliojihami wanaowalenga raia.
Mshahiri huyo maarufu ambaye pia ni mwanamuziki na msanii, alifanya kazi katika kituo kimoja cha redio mjini Mogadishu, ambako aliandika michezo ya kuigiza ya redio.
Michezo hiyo ilikosoa vikali kundi la wanamgambo la, Al-Shabaab.
Aidha alikosoa vikali kauli mbiu ya harakati za Al Shabaab na kusema kuwa inatoa taswira mbaya kuhusu dini ya kiisilamu.
Bwana Awale alikuwa maarufu sana miongoni mwa vijana waisilamu ambao walikuwa anawashawishi kupinga ghasia, na badala yake kutafuta elimu.
Chama cha kitaifa cha waandishi wa habari Somalia, kinaamini kuwa alilengwa kwa sababu ya kutoa maoni yake hadharani bila kuogopa.
Kulingana na chama hicho bwana Awale ni mwandishi wa kumi nane kuuawa nchini Somalia mwaka huu.

No comments: