SERIKALI kupitia mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA)
imetekezeza zaidi ya tani mbili za za vipodozi na vileo pamoja na juice, kutoka
nchi jirani za Zambia na Malawi lizizo ingizwa nchini kwa njia za panya na
wafanyabiashara wasio waaminifu.
Vipodozi hivyo viliteketezwa katika dampo la taka la mji
mdogo wa Tunduma wilayani Momba jijini Mbeya hivi karibuni na mamlaka hiyo
baada ya kuzimata mwaka jana katika mipaka za mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa wa afya mji mdogo Tunduma, Gerald Mlewa alisema kuwa wameteketeza jumla ya tani 2.7 za Vipodozi, Pombe kali na juisi ambavyo vyote vilikamatwa mwakajana katika msako wa mamlaka hiyo.
Alisema vitu hivyo vilivyo teketezwa viliingia nchini
bila kibali kutoka nchi jirani za Zambia na Malawi na vingine vikiwa ni vile
vilivyo na madhala kwa binadamu na kupigwa marufuku na Serikali.
Vitu hivyo vilikamatwa kutokana na kuingia nchini bila
kibari kitu ambachi ni kinyume cha sheria na kuanza kushamazwa na
wafanyabiashara wasio waaminifu na kuhatarisha afya za watanzania hasa watumiaji
wa vipodozi.
Alitaja baadhi ya bidhaa zilizo kamatwa na kuhifadhiwa na TFDA katika ghala la mji mdogo wa Tunduma kuwa ni pamoja na Carolite, Clare, Beta sol, Movate, Epiderm, Diploson, taint Claire, Wakuu, na Miss Afrika Zorro-creams.
Mbali na kuteketewa kwa vipodozi hivyo pia ziliteketezwa
pombe na juisi kutoka Malawi
na Zambia kama Double-Punch, Zed, Diamond, Savana na aina zingine za pombe kali ambazo hazijathibitishwa na Serikali.
na Zambia kama Double-Punch, Zed, Diamond, Savana na aina zingine za pombe kali ambazo hazijathibitishwa na Serikali.
Nae Mkaguzi mkuu wa TFDA Paulo Sonda alisema kuteketezwa
kwa bidhaa hizo ni kutokana na agizo kutoka kwa serikali kutokana na vipodozi
hivyo visivyofaa kwa matumizi ya binadamu.
Sonda alitoa wito kwa waagizaji na wafanyabiashara kuuza vipodozi au bidhaa ambayo zimehakikishwa na kupitishwa na mamlaka hiyo, kwa kuepuka kukamatwa au inakabiliwa na hatua za kinidhamu kutoka Serikali.
Kwa upande wake Naibu Meneja wa TFDA, Rodney Alananga alisema ukaguzi wa bidhaa katika mpaka itakuwa mara kwa mara na itakuwa inasimamiwa na Serikali kwa kusaidiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Polisi, Mahakama, maafisa Uhamiaji, Afya, kilimo.
Ofisi ya kituo cha msimamizi wa forodha mpakani Tunduma Raymond Mwanisawa alisema bidhaa hazifai zimekuwa zikiharibiwa katika Dumpo la taka la Mwaka ambazo zilikamatwa mwaka jana.
No comments:
Post a Comment