Sunday 17 August 2014

UWANJA WA NANENANE JIJINI MBEYA WA GEUKA KUWA GUBA LA TAKATAKA

 


Mazingira yalivyoacha baada ya kumalizikika maonyesho ya nanenane

karatasi zilivyosambaa




Ni kitambo sana tangu nilipofika katika eneo la Nane nane jijini Mbeya wakati huo kulikuwa na watu wengi sana hadi nikashangaa. Sikufahamu kuna kitu gani eneo hilo, lakini nilipouliza nikajibiwa kuwa kuna maonyesho ya Nanenane
. Ndipo nikafanya mpango kuingia. Nilipata shida mlangoni kutokana na kundi kubwa wa wananchi waliojitokeza kwenda kuangalia maonyesho ya nanenane, lakini nilijitahidi na nikalipa kiingilio ingawa ningeweza kuingia kwa kutumia kitambulisho cha kazi.
 Lengo langu lilikuwa kufahamu nini kinajili mlangoni wakati wa kuingia kwenye maonyesho hayo. Nikatoa shilingi mia tano na nikaruhusiwa kuingia. Ndani ya uwanja kulipendeza na mapambo mbalimbali nikawa nashangaa mabanda mbalimbali hamadi nikakutana ofisi moja iliyofahamika kwa jina la TASO. Nilifahamishwa kuwa wao ni wahusika wa uwanja huo na ndio wasimamizi wa mazingira yote nikafurahi nikawasifia walivyopendezesha mazingira. Baadaye niliondoka eneo hilo.
 Leo nimeamka asubuhi mapema na kuanza kufikiria mahali kwa kufanya matembezi. Nilichagua eneo la nanenane, ndipo safari ikaanza kuelekea viwanja kufika mlangoni sikukuta walinzi. Nikashangaa na kujiuliza leo vipi mbona hamna watu kama wale wala hamna kiingilio basi kama ilivyo kawaida ya kazi zetu nikajaribu kujua nini kinaendelea nikamwona mama nikamsalimia nikamuuliza swali.
 JOZ B: Mimi nimekuja matembezi mama ila nilichokiona kimenishangaza awamu iliyopita nilikuja hapa kulikuwa na watu wengi mlangoni wakiingia na kutoka huku wengine wakikusanya kiingilio leo wameenda wapi?
 MAMA:mwanangu hivi ndivyo inavyokuwa baada ya kumalizika kwa maonyesho ya nanenane mlangoni huwa tunaingia bila kiingilia pia hakuna biashara zinazoendelea humu ndani hivyo mwanangu ingia bila wasiwasi. 
 :Nikajikongoja kuingia viwanjani kama ilivyokuwa shabaha yangu , hamadi nilichokiona sikuamini nikajiuliza inamaana jalala limeamia huku nikizidi kushangaa nikapitiwa na nzi waliotoka kwenye uchafu nikaondoka kwa haraka nikizani nimeshinda wale nzi kufika mbele nikakumbana na makopo nikawazua mawazo nikakumbuka kuna kampuni niliikuta eneo hilo inamaana waliondoka bila kufanya usafi wa mazingira nikabaki bila jibu nikiangalia ile ofisi ambayo niliambiwa inashughulika na mazingira ya nanenane imefungwa nikakosa nikakosa wakumuuliza hilo hilo. 
Kwa mwonekano hule nikajiuliza je ingekuwa maonesho yanadumu kwa mwezi mzima? nadhani ningekuja na ndege ndogo kwasababu nafasi ya kupita ingekosekana.

Imeandaliwa na Joshua Chuwa

No comments: