Wakati harakati mbali mbali za
kukabiliana na ndoa na mimba za utotoni zikiendelea na hasa katika nchi
za Afrika, baadhi ya nchi barani humo zinakabiliwa na changamoto hiyo
kupita kiasi.
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya
Firauni.
Kesi ya kwanza na ya aina yake imefanyika na
hukumu yake kutolewa nchini
Ivory Coast baada ya mwanamume mmoja kumuoa binti yake wa umri wa miaka
11.
Kutokana na kitendo cha mwanamume huyo kumuoa
binti yake
alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya dola za Kimarekani
mia saba.
Mwendesha mashtaka Rosine Kone amesema kwamba
kesi hiyo
ya aina yake itatuma ujumbe mzito kwa raia wa nchi hiyo ili wanaume
waache tamaa.
Nao Umoja wa Mataifa unasema kwamba ndoa za
utotoni
nchini Ivory Coast si suala la kushangaza, kwani mmoja kati ya mabinti
watatu huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka kumi na nane.
credits kwa bbc
No comments:
Post a Comment