Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameitahadharisha
Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini kutorudia makosa yaliyokuwa
yanafanywa na Halmashauri kabla ya wakala huo kuanzishwa.
Amesema
kuwa matumizi mabaya ya fedha za barabara pamoja na barabara hizo
kujengwa chini ya viwango na kuisababishia serikali hasara ya kufanya
matengenezo ya mara kwa mara ni miongoni mwa changamoto ambazo serikali
imeamua kuzitafutia ufumbuzi kwa kuanzisha Wakala huo.
“Ukiitwa
Injinia na kazi yako iendane na cheo chako, sio unafanya kazi mpaka
hata sisi ambao hatuna ujuzi huo tukiona tunasema hii ipo chini ya
kiwango, na hapo mwanzo serikali ilikuwa inaelekeza pesa nyingi sana
kwenye barabara lakini kiuhalisia barabara hazipo na muda mwingine mvua
zinataka kuanza ndio utaona mkandarasi anaingia barabarani kwenda
kutengeneza barabara,” Mh. Zelote alifafanua.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Amesisitiza
kuwa kwa kuimarisha sekta ya barabara vijijini ndio miongoni mwa hatua
za kuuendea uchumi wa Viwanda ambao ndio kipaumbele cha serikali ya wamu
ya tano inayoongozwa na Mh. Dk. John Pombe Magufuli.
Hivyo
ametoa wito kwa wakala huo kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa uadilifu
na kuhakikisha mabadiliko yanaonekana na kuwaasa kuacha kufanya kazi kwa
mazoea na hatimae kurudisha nyuma azma ya serikali ya awamu ya tano.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) wakati
akifungua kikao cha bodi ya barabara, (katikati) Mkuu wa Wilaya ya
Sumbawanga Dk. Khalfan Haule pamoja na Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa
Bernard Makali.
No comments:
Post a Comment