Jeshi
la Polisi kanda maalum Dar es salaam limempa siku 3 tu Sheikh Issa
Ponda, ili kujisalimisha na kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, na
iwapo hatafanya hivyo watamchukulia sheria stahiki.
Tarifa
hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, na kusema kwamba ndani ya
siku hizo 3 lazima awe amekwenda kujisalimisha, la sivyo hatakuwa
salama.
“Ametenda
makosa ya jinai kama uchochezi, lakini pia amekuwa anatoa lugha ambazo
ni za kejeli, dhidi ya serikali, anatufutwa na kama unamjua mwambie
ajisalimishe ili tuweze kumhoji, kukimbia hakutomsaidia, tukiona kuna
kosa la jinai tutampeleka mahakamani kama hana tutamwachia, mimi nampa
siku tatu lakini akija leo ni nzuri zaidi, nampa siku 3 ajitokeze
mwenyewe aweze kuhojiwa, vinginevyo hatakuwa salama”, amesema Kamanda
Mambosasa.
Hapo
jana Jeshi la polisi lilivamia mkutano wa Sheikh Ponda aliokuwa nafanya
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, na kufanikiwa kukamata
baadhi ya watu wakiwemo waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye
mkutano huo.
No comments:
Post a Comment