Thursday 21 May 2015

TUME YA HAKI ZA BINADAMU YABAINI MAKOSA YA POLISI

 Tume ya haki za binadamu na utawala bora imebaini kuwa maafisa na askari polisi wa jeshi la polisi hawakuheshimu haki za binadamu na kuzingatia matakwa ya sheria zinazoongoza jeshi la polisi pamoja na uwepo wa udhalilishaji wa kijinsia wakati wa kukamata na kuwapeleka mahabusu wafuasi wa chama cha wananchi CUF katika tukio la maandamano ya January 27 mwaka huu. Taarifa ya uchunguzi ya tume hiyo ya haki za binaadamu na utawala bora iliyokuwa ikichunguza kubainia iwapo haki za binadamu zilivunjwa na taratibu kufuatwa pamoja na iwapo misingi ya utawala bora ilizingatiwa imetolewa na mwenyekiti wa tume hiyo Bahame Nyanduge na kubaini uwepo wa uvunjifu wa haki za binadamu pamoja udhalilishaji wakati wa kuwakamata waandamanaji pamoja na kutumia nguvu kubwa kupita kiasi iliyosababisha madhara hata kwa wasio husika na kulitaka jeshi hilo kutoa mafunzo kwa askari na maafisa wake kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora pamoja na kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari katika utekelezaji wa operesheni zake. Pia mwenyekiti huyo amelitaka jeshi la polisi lihakikishe maafisa na askari wak

No comments: