Baadhi
ya wabunge wameitaka serikali kutoa ufafanuzi baada kutenga kiasi
kidogo cha shilingi trilioni 5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo huku
trilioni 16 zikiwa zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya ofisi ikiwemo
vitafunwa wakati kunachangamoto nyingine zinazoikabili nchni ikiwemo
tatizo la maji, mikopo ya elimu ya juu pamoja na miundombimu ya barabara
katika baadhi ya maeneo.
Wakichangia mjadala wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2015/16 mbunge wa
viti maalum Pauline Gekul amesema haiwezekani, serikali kutenga trilioni
16 kwa ajili ya matumizi ya ofisi, huku inapunguza bajeti ya wizara ya
maji, ambapo mbune wa kinondoni Mhe. Idd Azzani akihoji serikali kutenga
bilioni 70 kwa ajili ya safari huku baadhi ya wanafunzi wanaotakiwa JKT
wamekwama kutokana na ukosefu wa fedha zisizozidi shilingi bilioni 10.
Wakati huohuo baadhi ya wabunge wameendelea kupinga hatua ya
serikali kupandisha tozo kwenye mafuta ya taa ili kuongeza fedha
zitakazosaidia kusambaza umeme vijini kwamadao kutaendelea kuwaumiza
wananchi wa hali ya chini, na kuwataka kuangalia uwezekano wa kutafuta
mapato kwenye mitandao ya siku za mkononi, huku wengine wakisisitiza
kuangalia uwezekano wa kuongeza kodi kwenye vinywaji ikiwemo bia ili
kupata fedha zitakazosaidia miradi ya maendeleo ikiwemo ya maji.
Aidha bunge linatarajia kuhitimisha mjadala kuhusu bajeti ya
serikali juni 23 mwaka huu ambapo serikali itatoa ufafanuzi wa hoja
zilizotolewa na wabunge kwa takribani siku saba za mjadala kabla ya
kupitishwa kwa bajeti ya mwaka 2015/16 ya jumla ya shilingi trillioni
22.495.2 ambapo kati ya fedha hizo shilingi trillioni 16 zimepangwa
kutumika katika shughuli za ofisi na trillioni 5 kutumia katika miradi
ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment