TP Mazembe imefanikiwa
kutwaa Kombe la DR Congo Super Cup kwa kuichakaza MK kwa mabao 7-0.
Watanzania Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu kila mmoja alipachika bao na kuisaidia timu hiyo kutwaa kombe.
Kwa mara ya kwanza, Samatta
aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania anayecheza ugenini kukabidhiwa kombe baada ya
fainali.
Samatta ndiye alikuwa
nahodha katika mchezo huo na kukabidhiwa mkononi kombe hilo ambalo aliliinua
juu kwa furaha kubwa na kuibua mayowe ya furaha kwa mashabiki we TP Mazembe.
No comments:
Post a Comment