MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kusini Mhe. David Kafulila amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Kigoma kujibu shitaka la kutumia lugha ya matumisi dhidi ya Mkuu wa Wilaya Uvinza Khadija Nyembo.
Kafulila alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa mbili asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Mbele ya Hakimu David Ngunyale,Wakili wa Serekali Marysinta Lazaro alidai kuwa Kafulila alitenda kosa hilo tarehe 1 mwezi wa 8 mwaka 2013 katika kata ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoani hapa.
Wakili Lazaro alisema kuwa Mbunge huyo alimtolea maneno machafu Mkuu wa Wilaya ya Uvinza kuwa hana maadili,ana akili finyu na ni kiumbe dhaifu kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani
Alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo namba cc6/205 umekamilika na kuomba kupangwa kwa tarehe nyingine kwaajili ya usikilizaji wa awali.
Hakimu Ngunyale alikubaliana na ombi hilo la wakili na kuiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 19 mei mwaka huu.
Kafulila alikana shtaka hilo na kukidhi masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho kutoka ofisi ya mtendaji wa kata na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni mbili.
Kabla ya kufikishwa mahakamni mbunge huyo alikuwa nje kwa dhamana ambayo alipewa na askari wa polisi kituo cha kati baada ya kuripotiwa kumtukana mkuu huyo wa Wilaya.
No comments:
Post a Comment