Tuesday 2 June 2015

Wahamiaji haramu 28 watiwa mbaroni nchini Algeria

Wahamiaji haramu 28 watiwa mbaroni nchini Algeria


Maafisa usalama wa Algeria wamesema kuwa, wahamiaji haramu 28 wametiwa mbaroni katika fukwe za nchi hiyo.

Shirika la habari la Ufaransa limewanukuu maafisa hao wakisema kuwa, askari wa ulinzi wa fukwe za Algeria wamekamata boti mbili katika bandari ya Annaba mashariki mwa Algiers, mji mkuu wa Algeria zikiwa na wahamiaji 28 haramu raia wa nchi tofauti na ambazo zilikuwa zinajiandaa kuelekea barani Ulaya kimagendo.
Askari hao wa Algeria wameongeza kuwa, watu waliokamatwa wana umri wa baina ya miaka 17 hadi 52 na walikuwa na lengo la kusafiri kimagendo kuelekea kwenye fukwe za kaskazini mwa bahari ya Mediterranean.

No comments: