makamu wa Rais wa Tanzania, Mohammad Gharib Bilal, amesema kuna haja ya elimu ya umma kutolewa mara kwa mara kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ili Watanzania wafahamu umuhimu wa jambo hilo.
Mohammad Gharib Bilal amesema kwenye hotuba yake kwa mnasaba wa siku ya mazingira duniani kwamba, Tanzania inakabiliwa na hatari ya kupoteza baadhi ya mimea na wanyama kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na watu wanaofuatilia maslahi yao binafsi. Ukataji miti ni moja ya matatizo aliyosema yanaipeleka pabaya Tanzania na kusisitiza kuwa hali hiyo isipodhibitiwa, matokeo yake yake yataviathiri vizazi vya sasa na vijavyo.
Kila mwaka, Juni mosi imetengwa kuwa siku ya mazingira duniani na serikali za dunia hutumia siku hiyo kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira. Umoja wa Mataifa umesema uharibifu wa mazingira ndio uliopelekea kutokea mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yameleta matokeo mabaya kama vile kushitadi ukame katika baadhi ya nchi na mafuriko katika baadhi ya zingine.

No comments:
Post a Comment