Kufuatia
mgogoro wa wakulima na wafugaji uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi
wilayani Mvomero mkoani Morogoro mahakama ya ardhi wilaya ya Morogoro
imefuta cheti cha usajili wa kijiji cha wafugaji kambala hukumu
iliosababisha mvutano mkubwa kati ya wakulima na wafugaji ambapo askari
wa jeshi la polisi walilazimika kuimarisha ulinzi katika mahakama ya
ardhi.
Wakulima na wafugaji wamefurika katika mahakama ya ardhi nyumba na
maendeleo ya makazi mjini Morogoro wakisubiri kusomwa kwa hukumu ambapo
akisoma hukumu hiyo mwenyekiti kiongozi wa baraza la ardhi Evelon
Muhava kutoka wilaya ya Dodoma amesema amelazimika kutoa hukumu kutokana
na kukamilika kwa ushahidi wa upande wa madai ya kijiji cha wafugaji
cha kambala na upande wa wadaiwa wakulima wa vijiji vya heberi ihombo
lukindo na wakulima wengine kutoka nje ya vijiji hivyo ambapo amesema
ili kumaliza mgogoro huo amefuta hati cheti cha usajili wa kijiji cha
kambala iliotolewa mwaka 2013 ambapo amesema imeonyesha kunamkanganyiko
kutoka na hati 1988 ya kijiji kuonyesha ukubwa wa kijiji ni hekta 16,104
wakati cheti kinaonyesha ukubwa wa kijiji ni hekta 48.65.
Aidha Muhava ameagiza mamlaka za ardhi na nyumba kuhakiki upya
mipaka ya kijiji cha kambala sambamba na kuanza kupima eneo lote la
bonde la mgongola kwa kushirikisha vijiji jirani vikiwemo vya Hembeti,
Dihombo, Mkindo na Kambala pamoja na kuweka bikon za kudumu katika
mipaka hiyo.
Wakizungumza nje ya mahakama hiyo wakulima wa ambao ndio wadaiwa
katika hukumu hiyo wamesema licha ya mahakama kutoa hukumu kwa
kuzingatia misingi ya haki lakini wameiomba serikali kuimalisha ulinzi
katika maeneo hayo wakati mamlaka zikitekeleza agizo la mahakama.
Kwa upande wao wafugaji ambao ndio wadai katika shauri hilo
wamesema hawakuelewa kabisa jinsi hukumu ilivyotolewa huku kwani
mahakama imetoa hukumu ya mipaka na si hukumu ya mgogoro.
No comments:
Post a Comment