Tuesday 23 June 2015

Waumini wa madhehebu ya dini morogoro wameitaka serikali kusimamia kwa haki zoezi la uandikishaji wapiga kura.


Waumini wa madhehebu ya dini mkoani Morogoro wameitaka serikali  kusimamia kwa haki zoezi la uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura kuhakikisha kila mwananchi mwenye sifa anaandikishwa  na anapata haki ya msingi ya kupiga kura na kuchagua viongozi .

Wakizungumza katika ibada ya maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa la Anglikan mkoani Morogoro waumini hao wamesema watanzania wanatakiwa kuchagua viongozi wenye hofu ya mungu na watakao idumisha amani ya Tanzania alio tuachia Bwana wetu Yesu Kristo ambapo wamewataka wakristo kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi serikalini katika chaguzi zijazo.
 
Kwa upande wao viongozi wa kanisa la Anglikani wa Dayosisi ya Morogoro Askofu Godfrey Sehaba amewataka wakristo kuwachagua viongozi wenye hofu ya mungu huku kaasisi wa kanisa la Anglikan Berega Aizack mgego amesema kuwepo kwa watangazania walio na elimu ya chini kuna sababishwa na viongozi wengi ambao wana elimu za juu kushindwa kuiongoza nchi katika haki na kuwapigania wanyonge.

No comments: