Wednesday 15 July 2015

AHUKUMIWA MIAKA 60 KWA KUWABAKA MAPACHA WENYE UMRI WA MIAKA TISA-KILOMBERO.



 
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Chita Wilayani Kilombero Bwana Abedy Jonathan Flana amehukumiwa kwenda jela miaka 60 na mahakama ya Wilaya ya Kilombero kwa kosa la kuwabaka watoto wawili ambao ni mapacha wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji hicho.
Hukumu hiyo imetolewa july 15 mwaka huu na hakimu Bigirwa Nyakato baada ya mahakama kujiridhisha na pasipokuacha shaka lolote na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka Mkaguzi wa Polisi Joseph Elias Isagala ameiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Aprily 20 mwaka 2014Bwana Abedy Flana ametenda kosa hilo,baada ya kuwahadaa kwa kuwapa matunda ya maparachichi.

Bwana Isagala ameiambia mahakama kuwa mnamo April 20 mwaka 2014 watoto hao walitumwa na wazazi wao kwenda kufukuza ndege mashambani Bwana Abedy akawafuata na akawaambia kuwa waende kuangua maparachichi na walipoangua akawaambia anataka kufanya nao mapenzi huku akiwatisha wasiseme kwa mtu yeyote na atakayetoa taarifa hiyo atamuua
Aidha baada ya kuwatisha huku akiendelea kuwalubuni na hatimaye akatekeleza unyama huo ambapo baada ya kuwabaka aliwasabaishia mamumivu makali sehemu zao za siri hali iliyowafanya washindwe kutembea vizuri.

Mapacha hao wenye umri wa miaka tisa wakiwa ni wanafunzi wa darasa la tatu waliporudi nyumbani majira ya jioni wazazi baada ya kuona watoto hao wanashindwa kutembea vizuri ndipo walipowachunguza sehemu zao za siri na kukuta zimeharibiwa vibaya na kuchukua hatua ya kwenda kuripoti police na hatimaye wakapewa fomu namba tatu kwa ajili ya matibabu.
Baadae wakawapeleka zahanati ya chita na baadae kituo cha Afya Mngeta ambapo wakawarufaa hadi Hospitali ya Mtakatifu Fransisco na baada ya kupatiwa matibabu mtuhumiwa alikamatwa April 21 mwaka 2014 na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kubaka watoto wawili April 30,2014.
Hata hivyo mahakama baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka imemuhukumu mika 30 kwa kila kosa ambapo sasa atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka 60 jela.
Hakimu Bigirwa amesema Mahakama imetoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia na mienendo kama hiyo kwani makosa ya ubakaji yamekua sugu kwenye jamii,hivyo jamii inapaswa kujirekebisha

No comments: