Wednesday 5 August 2015

Wanachama wa CUF wamezingira ofisi za Chama Hicho Wakitaka Kujua hatima ya Prof.Ibrahim Lipumba Aliyedawai kutaka Kujiuzulu


Leo ilikuwa Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim azungumze na Wanahabari asubuhi, ila mkutano huo umehairishwa hadi siku nyingine tena.
 
Wanachama wa chama cha wananchi CUF walizingira ofisi za chama hicho wakiongozwa na wazee wakitaka kujua hatima ya mwenyekiti wao Prof.Ibrahim Lipumba aliyedawai kutaka kujiuzulu.
Magdalena Sakaya alipoulizwa Prof. Lipumba alitaka kuzungumza nini amejibu hata  wao hawajui kitu alichotaka kuwaambia wananchi  
 
Magdalena alisema sababu kubwa ya kusitishwa mkutano  huo ni kuwa  Wazee wa CUF wametaka kujua kwanza ni kitu gani Mwenyekiti anataka kuongea.
 
Wananchi nje ya ofisi za CUF walikuwa wanashangilia wakiimba kwa kusema..... "Si mnaona, muziki wa Lipumba kuuzima hamuwezi"
 
Mmoja wa Wananchi waliokuwa wanashangilia alisema wamefurahia kwakuwa wanaamini Mwenyekiti wao Lipumba hatajiuzulu na yuko na wananchi.

No comments: