Wednesday 13 April 2016

Polisi watatu Wafikishwa Mahakamani Wakituhumiwa Kupokea Rushwa


Polisi watatu wa wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa. 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, iliwafikisha askari hao jana katika Mahakama ya Wilaya ya Urambo huku mwingine akidaiwa kukimbia.

Askari hao waliofukuzwa kazi kabla ya kufikishwa mahakamani ni John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robart. 

Anayedaiwa kukimbia ni Elisha ambaye polisi inaendelea kumtafuta. 

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Urambo, Hassan Momba, Wakili wa Takukuru, Edsoni Mapalala alidai washitakiwa walitenda makosa hayo Machi 7 mwaka huu.

Mapalala alidai siku hiyo katika kijiji cha Mkirigi, Kata ya Ilege, Wilaya ya Kaliua, washitakiwa hao wakiwa waajiriwa wa jeshi la polisi, waliomba rushwa ya Sh milioni tatu kutoka kwa Dotto Gandulanye ili wasimchukulie hatua za kisheria baada ya kumkuta akiwa na bangi.

No comments: