Wednesday, 15 July 2015

PROF. MARK JAMES MWANDOSYA AWASHUKURU WOTE WALIOMUUNGA MKONO KABLA NA BAADA YA KUTANGAZA NIA.


Profesa Mark James  Mwandosya 
" Katika nyakati mbalimbali mataifa, na binadamu pia hupita katika vipindi vya majaribu (testing times). Majaribu hayo ni njia moja ambayo naamini Mwenyezi Mungu, muweza wa yote, humuimarisha mtu na huimarisha Taifa iwapo tunaweza kuyamudu". 

Hiki ndio kipindi tunachopita sasa kama Taifa. Kwa maneno hayo napenda, kwa unyenyekevu mkubwa, kuwashukuru, na kwa dhati kabisa, wale wote mliotuunga mkono kabla na baada ya kutangaza nia, wakati wa na baada ya kuchukua fomu za kuomba nafasi hiyo, kwa imani kwamba tunakidhi, na pengine tunazidi vigezo vilivyoorodheshwa.

 Mliotudhamini kwa matumaini makubwa, mliotusaidia, kwa hali na mali kufanikisha zoezi la kupata wadhamini, na wengi mliotuletea, kwa njia mbalimbali, ujumbe wa kutuunga mkono, tunawashukuru.  Haikuwa kama tulivyotarajia, na mlivyotarajia. 

Kila tukio lina maana yake katika maisha. Hatimaye ukweli unabakia kwamba Taifa ni kubwa kuliko nafsi na utashi wetu kama mtu mmoja mmoja. Asanteni Kaskazini Pemba, Kusini Pemba, Kaskazini Unguja, Mjini Unguja, Magharibi Unguja, Kusini Unguja, na Tanzania Bara, kutoka Tanga mpaka Katavi, na kutoka Kagera mpaka Mtwara. Mbeya, nawashukuru. Mmenilea na hivyo kunifanya hatimaye nitoe utumishi kwa nchi yetu tunayoipenda. Rungwe,na mahsusi Rungwe Mashariki (Busokelo), mmeniamini na siku zote mmenipa ushirikiano uliotuwezesha kufanya yale mengi tuliyoyaweza. Ndugu na marafiki zangu na wenzangu katika utumishi wa umma, kwa ujumla wenu, nawashukuru. 

Asanteni sana. Familia yangu daima imekuwa ngome yangu katika maisha. Nitaendelea kutoa mchango wangu kwa Taifa kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyoniwezesha. Kiswahili hakijasheheni katika istilahi, hasa pale unapotaka kutoa maneno ya shukrani kutoka zsakafu ya moyo. 

Yatosha kusema ASANTE SANA."-Prof. Mark James MwandosyaIssa, nitashukuru kama utaiweka makala hii fupi.Asante sana.Mwandosya." Katika nyakati mbalimbali mataifa, na binadamu pia hupita katika vipindi vya majaribu (testing times). Majaribu hayo ni njia moja ambayo naamini Mwenyezi Mungu, muweza wa yote, humuimarisha mtu na huimarisha Taifa iwapo tunaweza kuyamudu. Hiki ndio kipindi tunachopita sasa kama Taifa. 


Kwa maneno hayo napenda, kwa unyenyekevu mkubwa, kuwashukuru, na kwa dhati kabisa, wale wote mliotuunga mkono kabla na baada ya kutangaza nia, wakati wa na baada ya kuchukua fomu za kuomba nafasi hiyo, kwa imani kwamba tunakidhi, na pengine tunazidi vigezo vilivyoorodheshwa. Mliotudhamini kwa matumaini makubwa, mliotusaidia, kwa hali na mali kufanikisha zoezi la kupata wadhamini, na wengi mliotuletea, kwa njia mbalimbali, ujumbe wa kutuunga mkono, tunawashukuru.  Haikuwa kama tulivyotarajia, na mlivyotarajia. Kila tukio lina maana yake katika maisha.

 Hatimaye ukweli unabakia kwamba Taifa ni kubwa kuliko nafsi na utashi wetu kama mtu mmoja mmoja. Asanteni Kaskazini Pemba, Kusini Pemba, Kaskazini Unguja, Mjini Unguja, Magharibi Unguja, Kusini Unguja, na Tanzania Bara, kutoka Tanga mpaka Katavi, na kutoka Kagera mpaka Mtwara. Mbeya, nawashukuru. Mmenilea na hivyo kunifanya hatimaye nitoe utumishi kwa nchi yetu tunayoipenda. Rungwe,na mahsusi Rungwe Mashariki (Busokelo), mmeniamini na siku zote mmenipa ushirikiano uliotuwezesha kufanya yale mengi tuliyoyaweza. 

Ndugu na marafiki zangu na wenzangu katika utumishi wa umma, kwa ujumla wenu, nawashukuru. Asanteni sana. Familia yangu daima imekuwa ngome yangu katika maisha. Nitaendelea kutoa mchango wangu kwa Taifa kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyoniwezesha. Kiswahili hakijasheheni katika istilahi, hasa pale unapotaka kutoa maneno ya shukrani kutoka zsakafu ya moyo. Yatosha kusema ASANTE SANA."-Prof. Mark James Mwandosya

No comments: