Monday 3 October 2016

Watu watatu waamefariki dunia baada ya kutokea ajali ya barabarani oktoba 2

Watu watatu waamefariki dunia baada ya kutokea ajali ya barabarani oktoba 2 mwaka huu majira ya saa moja usiku barabara ya TANZAM Mbeya kwenda Tunduma eneo la Chimbuya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe. Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Mathias Nyange amesema kuwa ajali hiyo umehusisha gari aina ya Coaster yenye namba za usajili T 181 DCJ ambapo dereva wake hajafahamika na alitoroka baada ya ajali kuigonga pikipiki namba MC 445 EFD iliyokuwa inaendeshwa na Julius Mfiao mkazi wa kijiji cha Mponela Kata ya Isandula Wilaya ya Mbozi akiwa amepakia abiria wawili ambao nao walifariki papo hapo. Nyange amewataja abiria waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Oid Msukwa na Iddy Siwelwe wote wakazi wa Kijiji cha Mponela Kata ya Isandula Wilaya ya Mbozi. Kamanda Nyange amesema chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa ikiwa ni pamoja na kumtafuta dereva wa gari aina ya Coaster. Aidha miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi wakati taratibu za kuwakabidhi ndugu zikiwa zinaendelea. Hata hivyo Nyange ametoa wito kwa madereva kufuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuonya madereva wa pikipiki kuacha kupakia abiria zaidi ya mmoja na kwamba Jeshi lake halitasita kuwachukulia hatua watakaokwenda kinyume cha sheria. Na Ezekiel Kamanga

No comments: