Tuesday 29 May 2018

Mfaransa Simba ataka Mil 90 kwa mwezi

Kocha wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre kwa sasa analipwa mshahara wa Sh.45 milioni kwa mwezi na Mtunisia, Aymen Habib Mohammed anachukua Sh 23 milioni kwa mwezi lakini kama Simba itabadili mawazo na kumpa mkataba mpya sharti lake la kwanza ni mshahara kupandishwa kwa asilimia 100.
Hiyo inamaanisha kwamba kama viongozi wakikubaliana na matakwa ya nyongeza zao Lechantre atalipwa Sh 90 milioni na Aymen atapokea Sh 45 milioni, hiyo ni tofauti kabisa na malazi, usafiri na posho zao.
Lakini katika usafiri wa ndege popote pale wanapokwenda nje ya nchi wanataka tiketi ya daraja la kwanza ambayo ni ghali zaidi ya ile ya kawaida.

No comments: