Tuesday 2 October 2012

AJALI MBALIZI MBEYA...WATU KUMI WAFARIKI DUNIA


MBUNGE VITI MAALAM MBEYA DR.MARY MWANJELWA AKIWA HOSPITlLI YA FISI BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA.

UP DATE YA AJALI MBALIZI MBEYA.. MBUNGE DR.MWANJELWA ANUSURIKA KUFA

 HII NDIYO GARI ALIYOKUWEMO MBUNGE MARY MWANJELWA, HAPA NI MBALIZI IKIWA IMETEKETEA KWA MOTO.



 

·       Ajali mbaya yatokea Mbalizi Mbeya
·       Katibu wake ateketea kwa moto, ni zaidi ya watu watano
 Na, Gordon Kalulunga, Mbeya
MBUNGE wa viti maalum mkoani Mbeya kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dr. Mary Mwanjelwa, amenusurika kufa katika ajali mbaya iliyotokea jana eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa baada ya gari lake kugongwa na kuteketea kwa moto.
Ajali hiyo imehusisha magari Manne likiwemo Lori la Mafuta kampuni ya lake Oil lenye namba za usajili T 814 BTC , gari ndogo ya abiria (Hiace) yenye namba za usajili T 299 BCE na gari ya Mbunge huyo Mary Mwanjelwa Toyota Hilux T 671 ABM
Watu zaidi ya saba walifariki papo hapo huku wengine miili yao ikiwa imeteketea vibaya kwa mota baada ya gari hizo kugongana kisha kulipuka.
Mashuhuda wa ajali hiyo wakiwemo majeruhi, walisema Petro Tank iliyokuwa imebeba mafuta, iliferi breck katika mteremko wa Mlima Iwambi kisha kuliparamia Lori lingine na kuigonga gari ya Mbunge Mwanjelwa kisha kuvaana uso kwa uso na gari ya abiria iliyokuwa ikitokea eneo la Mbalizi.
 kalulunga blog kilishuhudia mtu aliyeongoza uokojai ambapo alikuwa ni Koplo Mathias Joachim wa  Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania 44 KJ Mbalizi Mbeya Karume Camp.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alifika eneo la tukio na ametoa pole kwa wafiwa kisha ameelekea Hospitali ya Ifisi Mbalizi kwa ajili ya kuwajulia hali majeruhi akiwemo Mbunge huyo.
Mbunge Mary Mwanjelwa, akiwa Hospitalini hapo alimshukuru Mungu kwa kumnusuru kisha akauliza kama dereva wake anayejulikana kwa jina la Rajab na katibu wake Muhtasi Amina ambapo aliambiwa kuwa wapo Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Dereva wake Mr. Rajabu ambaye alipelekwa katika Hospitali hiyo ya Ifisi, ameumia vibaya kichwani na miguu yote miwili huku katibu wa Mbunge huyo imesemekana kuwa amekufa kwa kuteketea kwa moto ndani ya gari hiyo.
Kati ya zaidi ya watu saba ambao wamefariki katika ajali hiyo yumo askari Polisi wa kituo kidogo cha Mbalizi aliyetajwa kwa jina la PC Samson.
Kikosi kazi cha mtandao huu wa kalulunga.blogspot.com kinatoa pole kwa wafiwa wote na Mungu awasaidie majeruhi wapone haraka kwa ajili ya kuendelea kulijenga Taifa letu la Tanzania.

 HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
 MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
 HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI
 HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA 
 FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO
 ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKA ENEO LA TUKIO AMBAPO MAGARI HAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATU KUMI.
 WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI
 HUU NDIO MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE
 HAYA NI MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALO LILIUNGUA LOTE
WANANCHI MBALI MBALI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA WALIO PATA AJALI

BREAKING news........AJALI YA PETRO TANK LAPINDUKA MBALIZI MBEYA NA LINAWAKA MOTO MUDA HUU

STENDI YA MABASI MBALIZI YAANZA KUJENGWA KWA KIWANGO CHA KISASA

No comments: