Wednesday, 31 October 2012

MEMBE: HAKUNA MTU KUSEMA ZIWA LOTE NI LAKE.

WAZIRI MEMBE AKIWA KATUMBASONGWE.
Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiongea na wazee waishio Katumbasongwe, kando ya Ziwa Nyasa ndani ya Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.
Wakazi wa Katumbasongwe walimiminika kwa wingi kumsikiliza Mhe. Membe.
Wazee wa Katumbasongwe wakinyoosha mikono kujitambulisha umri wao wakati wa Mkutano wao na Waziri Membe uliofanyika jana Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.  Waziri Membe alikuwa Mkoani humo kwa ziara ya siku mbili ambapo alitembelea maeneo na makazi ya wananchi waishio ufukweni mwa Ziwa Nyasa.
WAZIRI MEMBE AKIWA MATEMA
Waziri Membe akiongea na wakazi wa Matema, Wilayani Kyela ambapo aliwasihi waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo.  Aidha, Mhe. Membe alisema Serikali inajitahidi kadri iwezavyo kutafuta suluhisho la mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi. 
Wakazi wa Matema, waishio katika ufukwe wa Ziwa Nyasa, Wilayani Kyela wakimsikiliza Waziri Membe alipowatembelea jana.
Waziri Membe (hayupo pichani) pia alipata fursa ya kuongea na wazee wa Matema ikiwa ni sehemu ya mwisho wa ziara yake ya siku mbili Mkoani Mbeya.  Katika mazungumzo yake na wazee hao, Waziri Membe aliwaeleza kuwa ziara hii ni sehemu ya kukusanya ushahidi muhimu kutokana na maelezo ya historia watakazochangia hususan tangu enzi ya ukoloni kuhusu Ziwa Nyasa.

No comments: