Uamuzi huo wa Azam umekuja siku moja baada ya kukatisha mkataba wake na kocha Boris Bonjuk raia wa Serbia ambaye ameinoa timu hiyo kwa siku 84 tu.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Stewart kuonoa timu hiyo kabla ya uongozi wa klabu kukatisha mkataba wake kwa madai timu haina mabadiliko pamoja na kuwasaidia kuchukua nafasi ya pili katika ligi kuu msimu uliopita.
Afisa Habari wa Azam Jaffar Idd alisema kuwa kocha huyo anawasili nchini leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi ya kuinoa timu hiyo.
Alisema uamuzi huo umechukuliwa na uongozi wa klabu ya Azam baada ya kutoliridhishwa na kiwango cha kocha wao Bonjuk toka aanze kazi.
Alisema mapendekezo ya kumsimamisha Bonjuk yamefanywa na uongozi kutokana na mapendekezo ya wataalamu wa ufundi na wadau mbali mbali wa soka.
Stewart anarejea huku Azam wakiwa na mechi ngumu mbele yao ikiwemo ya Coastal Union Kesho na Yanga Jumapili.
Habari ambazo zilipatikana jana zilieleza kuwa Azam wamekatisha mkataba wa Stewart na Sofapaka ambao waliiingia nao hivi karibuni baada ya kuondoka Azam.
Azam wa amekatisha mkataba na Bonjuk kwa madai kuwa timu haichezi mpira wa pasi kama awali walivyokuwa na Stewart bali wanacheza mpira wa butua butua usiokuwa na malengo kitu kinachopelekea ushindi mdogo katika mechi zao.
Pamoja na kumtimua kocha huyo lakini Azam mpaka sasa wamecheza michezo 9 wamepoteza mchezo mmoja dhidi ya Simba kwa kufungwa bao 3-1.
Hii itakuwa ni mara ya pili uongozi wa klabu ya Azam kuchukua hatua ya kuwafukuza makocha wake pindi wanapofungwa na Simba.
Katika mchezo wa Ngao ya Hisani waliocheza Taifa Simba na Azam na kumalizaka kwa ushindi wa bao 3-2 waliopata Simba ndipo Uongozi ulimfukuza Stewart kwa madai kuwa alimchezesha Mrisho Ngassa katika mechi hiyo huku uongozi walisema asipangwe.
tewart Hall ambaye anatua leo nchiki akitokea Kenya kwa ajili ya kuanza kazi rasmi katika klabu hiyo.
Uamuzi huo wa Azam umekuja siku moja baada ya kukatisha mkataba wake na kocha Boris Bonjuk raia wa Serbia ambaye ameinoa timu hiyo kwa siku 84 tu.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Stewart kuonoa timu hiyo kabla ya uongozi wa klabu kukatisha mkataba wake kwa madai timu haina mabadiliko pamoja na kuwasaidia kuchukua nafasi ya pili katika ligi kuu msimu uliopita.
Afisa Habari wa Azam Jaffar Idd alisema kuwa kocha huyo anawasili nchini leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi ya kuinoa timu hiyo.
Alisema uamuzi huo umechukuliwa na uongozi wa klabu ya Azam baada ya kutolirishwa na kiwango cha kocha wao Bonjuk toka aanze kazi.
Alisema mapendekezo ya kumsimamisha Bonjuk yamefanywa na uongozi kutokana na mapendekezo ya wataalamu wa ufundi na wadau mbali mbali wa soka.
Stewart anarejea huku Azam wakiwa na mechi ngumu mbele yao ikiwemo ya Coastal Union Kesho na Yanga Jumapili.
Habari ambazo zilipatikana jana zilieleza kuwa Azam wamekatisha mkataba wa Stewart na Sofapaka ambao waliiingia nao hivi karibuni baada ya kuondoka Azam.
Azam wa amekatisha mkataba na Bonjuk kwa madai kuwa timu haichezi mpira wa pasi kama awali walivyokuwa na Stewart bali wanacheza mpira wa butua butua usiokuwa na malengo kitu kinachopelekea ushindi mdogo katika mechi zao.
Pamoja na kumtimua kocha huyo lakini Azam mpaka sasa wamecheza michezo 10 wamepoteza mchezo mmoja dhidi ya Simba kwa kufungwa bao 3-1.
Hii itakuwa ni mara ya pili uongozi wa klabu ya Azam kuchukua hatua ya kuwafukuza makocha wake pindi wanapofungwa na Simba.
Katika mchezo wa Ngao ya Hisani waliocheza Taifa Simba na Azam na kumalizaka kwa ushindi wa bao 3-2 waliopata Simba ndipo Uongozi ulimfukuza Stewart kwa madai kuwa alimchezesha Mrisho Ngassa katika mechi hiyo huku uongozi walisema asipangwe.
No comments:
Post a Comment