>>CAPITAL ONE CUP UWANJA: Stamford Bridge JUMATANO SAa 4:45 Usiku
Sir
Alex Ferguson amemtakia kila la heri Refa Lee Mason katika Mechi ya
Jumatano Oktoba 31 itakayochezwa Uwanja wa Stamford Bridge kati ya
Chelsea na Manchester United ikiwa ni Mechi ya Raundi ya 4 ya Mtoano ya
CAPITAL ONE CUP ambayo imekuja Siku 3 tu baada ya Timu hizo kupambana
kwenye Ligi na Chelsea kuchapwa 3-2 huku Wachezaji wao wawili kutolewa
kwa Kadi Nyekundu na wao kubakia kuwasilisha malamiko rasmi kwamba Refa
wa Mechi hiyo, Mark Clattenburg [Pichani], alitumia lugha isiyofaa dhidi
ya Wachezaji wao.
Kwa sasa FA, Chama cha Soka cha England,
kimefungua uchunguzi kuhusu tuhuma hizo dhidi ya Refa Clattenburg na
wakati huo huo Polisi nao wanafanya uchunguzi wao kuhusu Refa huyo baada
ya kupokea malalamiko kutoka Kundi la Wanasheria Weusi kuhusu tuhuma za
Ubaguzi za Refa huyo dhidi ya Kiungo wa Chelsea John Mikel Obi na Juan
Mata.
Vile vile, Polisi wanachunguza kuumizwa
kwa Mlinzi wa Uwanja na Mashabiki wa Chelsea waliporusha vitu Uwanjani
kumtupia Javier Hernandez aliekuwa akisherehekea kufunga bao la 3 na la
ushindi.
Akiongea na Wanahabari kuhusu Mechi ya
CAPITAL ONE CUP na Chelsea, Sir Alex Ferguson aliulizwa kama ana ujumbe
wowote kwa Refa Mason, Ferguson alijibu: “Namtakia bahati njema Refa!”
Ni wazi, hasa baada ya matukio ya Mechi
ya Jumapili ambayo Chelsea iliwapoteza Branislav Ivanovic na Fernando
Torres kwa Kadi Nyekundu, Refa Lee Mason atakuwa akiaangaliwa kwa makini
kuhusu uchezeshaji wake.
Akiongelea Timu yake, Sir Alex Ferguson
amesema atabadili Wachezaji na huenda Nani, Chicharito, Ryan Giggs,
Anderson, Paul Scholes na Danny Welbeck wakacheza pamoja na Chipukizi
Scott Wootton, Belgian Marnick Vermijl, Michael Keane na Nick Powell.
Hata Chelsea watalazimika kufanya
mabadiliko kwa vile Ivanovic, Torres na John Terry wapo Kifungoni na
Frank Lampard ni majeruhi.
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP
RATIBA RAUNDI ya 4:
Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu
Jumanne Oktoba 30
Sunderland v Middlesbrough
Swindon v Aston Villa
Wigan v Bradford
Leeds v Southampton
Reading v Arsenal
Jumatano Oktoba 31
Norwich v Tottenham
Liverpool v Swansea [SAA 5 Usiku]
Chelsea v Manchester United
No comments:
Post a Comment