Tuesday, 30 October 2012

Messi atunzwa BUTI ya DHAHABU Ulaya!


Chapisha Toleo la kuchapisha
LIONEL_MESSIStaa wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi, ametunzwa Kiatu cha Dhahabu, hii ikiwa ni mara yake ya pili, kwa kufunga Bao nyingi katika Ligi Msimu uliopita.
Messi, Miaka 25, aliweka rekodi huko Spain kwa kuifungia Bao 50 Barcelona na kumpiku Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kwa Bao 4.
Akipokea Tuzo hiyo, Messi alisema: “Hii ni zawadi kwa kufunga Mabao lakini bila Wachezaji wenzangu nisingefunga. Kwa hiyo hii ni zawadi yetu wote!”
Messi alitwaa Buti ya Dhahabu kwa mara ya kwanza Mwaka 2010 kwa kufunga Bao 34 na kuisaidia Barcelona kutwaa Ubingwa.
Messi, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, pia yumo kwenye Listi ya Wagombea Tuzo ya FIFA ya 2012 ya Ballon d'Or ambayo hutunukiwa Mchezaji Bora na yeye ni miongoni mwa Wachezaji 23 watakaoiwania.
Kocha wa Barcelona, Tito Vilanova alisema: “Hatutaona Mchezaji mwingine kama yeye! Si kwa magoli anayofunga bali kwa jinsi anavyouelewa mchezo ndilo linamfanya awe bora! Jumamosi, alikimbia Mita 50 kurudi nyuma kusaidia ulinzi wakati wa kona wakati tunaongoza bao 5-0! Si Wachezaji wengi wangefanya hivyo!”
Messi alikabidhiwa Tuzo hiyo ya Buti ya Dhahabu na Luis Suarez Miramontes ambae ni Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Spain alieshinda Ballon d'Or Mwaka 1960.

No comments: