Tuesday, 30 April 2013

ASKARI MWANAUME ABAKWA NA WANAWAKE WANNE BAADA YA KUTEKWA


Askari mmoja mwanaume anadaiwa kutekwa kisha kudhalilishwa kijinsia na wanawake wanne kwa karibu wiki moja kabla ya kupigwa mawe na kutupwa katikati ya milima.

Mateso ya muathirika huyo mwenye miaka 25 yalianza pale alipopata lifti ya gari kuelekea mji wa Mutare nchini Zimbabwe.
Wanawake wawili na mwanaume mmoja walikuwa kwenye gari, Mercedes Benz, na, baada ya kuendesha kwa takribani saa moja kuelekea mji huo, dereva wa gari hilo akabadili mwelekeo wa safari hiyo.
Ndipo muathirika huyo akalalamika, alitishiwa kwa kisu.
Msemaji wa polisi wa Manicaland, Inspekta Msaidizi Nuzondiwa Clean, alieleza: "Baada ya kubadilishwa mwelekeo huo, mlalamikaji alihoji wapi walikokuwa wakielekea na walimweleza walikuwa wakienda kupata chakula.
 
"Askari huyo alitaka kushushwa, lakini dereva huyo akatoa kisu na kumtishia nacho. Mmoja wa abiria wanawake akamfunga kwa kitambaa cheusi machoni mtuhumiwa huyo."
 Kwa mujibu wa Nuzondiwa,watesi  hao  walimpeleka mlalamikaji kwenye nyumba isiyojulikana ambako walimvua nguo zote na kumpora simu yake na Dola za marekani 35.
 Watuhumiwa walimwamuru mtu huyo kulala na mmoja wa wanawake hao katika matukio kadhaa na alishikiliwa kati ya Aprili 19-23.
 
 Kisha akafungwa tena kitambaa machoni na kushushwa kwenye Milima ya Dangamvura ambako, kwa mujibu wa polisi, alipigwa mawe katika mguu wake wa kushoto, na kumsababishia majeraha makubwa.
 Watuhumiwa hao kisha wakawasha gari lao na kutokomea kusikojulikana.Askari huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Sakubva

No comments: