Saturday 13 April 2013

SHULE ZA SEKONDARA ILEJE KUPATIWA MAABARA RAFIKI


HALMASHAURI ya Wilaya ya Ileje mkoani hapa imetumia kiasi cha shilingi
milioni 35,880,000 kwa ajili ya ununuzi wa Maabara rafiki sita
ilikuondokana na tatizo lililo kuwa linaikabiri la mafunzo ya vitendo
kwa masomo ya Sayansi.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo Rosemary Senyamule wakati
wa makabidhiano ya maabara hizo na Kampuni ya Mlenterprises (LTD)
amabapo alisema kuwa tatizo la wanafunzi kusoma bila mafunzo ya
vitendo litakuwa limepungua.

Alisema kuwa juhudi za kununua maabara hizo ni kutokana na Halmashauri
hiyo kuhakikisha wanafunzi wanapata mafunzo ya vitendo na kuwa hela
hizo zilikuwa zimetorewa na Serikali kwa ajili ya kazi za wilaya hiyo
na wakaamua kununua maabara hizo.

Senyamle aliongeza kuwa halmashauri hiyo inaishukuru serikari kwa
kuweza kuwapatia fedha hizo kwa kuwa imesaidia kuondokana na tatizo
ambalo lilikuwa linaikumba wilaya hiyo kwa muda mrefu wanafunzi
hawajawahi kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo.

Naye Afisa elimu wa Sekondari Jimmy Nkwamu alisema kuwa katika
halmashauri hiyo hakujawahi kuwepo kwa maabara hizo na kuwa kwa sasa
kutasaidia kupunguza tatizo la wanafunzi kuferi masomo ya sayansi kwa
kuwa watafanya kwa vitundo.

Nkwamu alizitaja shule zilizo pewa maabara hizo kuwa ni sekondari ya
Lubanda, Ngulilo, Ikinga, Ibaba, Itale na Ileje day na kuwa zingine
zitapatiwa baada ya kununua maabara nyingine ama kuazimishana kwa
shule zote wilayani humo.

Alisema kuwa sifa za maabara hizo zinaweza kuhamishwa kutoka shule
moja kwenda shule nyingine na kuwa saizi wanafunzi watakuwa na uelewa
mkubwa kwa masomo hayo zaidi kwa vitendo na kuongeza ufanisi zaidi.

Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ibaba Emeka Minga alisema kuwa
kupata kwa maabara hizo katika wilaya hiyo na hususa ni kwa shule yake
kutawasaidia wanafunzi hao kujifunza kwa vitendo zaidi.

Alisema kuwa katika uajili wake aliokuwa ameajiliwa halmashauri ya
wilaya hiyo hajawahi kuona maabara hizo na kuwa kwa sasa wanafunzi
watakuwa na uelewa zaidi kuliko ilivyo kuwa mala ya kwanza ambapo
walikuiwa hawana vifaa hivyo.

Kwa upande wake mwanafunzi wa shule ya Itale Robert Ndidi alisema kuwa
kupatikanika kwa maabara hizo kumewasaidia kufundishwa kiulahisi kwa
vitendo zaidi kwa masomo ya sayansi na kuwa uelewa utazidi kwa
wanafunzi wilayani humo.

No comments: