KIKAO Cha dharura cha baraza la madiwani kilichoketi mwishoni
mwa wiki iliyopita kilimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela
Mkoani Mbeya kumfikisha mahakamani Afasa mtendaji wa kijiji cha Ipinda Boniface
Kayuni kutokana na kosa la wizi wa feddha linalomkabili.
Akizungumza katika kikao hicho mwenyekiti wa Halmashauri
ya wilaya Gabriel Kioija alisema Afisa huyo anayetuhumiwa kwa kosa la kufoji
kaboni sleep katika risiti na kujipatia fedha Tsh,3,42,000 kinyume cha taratibu
huku akiikosesha mapato Halmashauri,
Kipija alisema kuwa kutokana na kosa hilo Halmashauri iliunda tume kwa lengo la kuchunguza
tuhuma hizo ambapo tume hiyo ilibaini ukweli wa kosa hilo
na kupeleka vielelezo hivyo kwenye baraza hilo
ambalo tayari limemtaka Mkurugenzi huyo ampeleke mahakamani ili sheria ichukue
mkondo wake,
‘’Kutokana na ushahidi na
nvielelezo tulivyovipata kutoka katika tume ya uchunguzi umeonekana kuwa Afisa
huyo mtendji amekuwa na tabia ya kutenda kosa kama hilo mara kwa mara na kujipatia
fedha kinyume na taratibu huku akiikosesha fedha Halmashauri hivyo sisi kama
madiwani hatuko tayari kufanya kazi na mtu wa namna hiyo,tunakuamuru mkurugenzi
umpeleke mahakamani ili sheria ifanye kazi yake,’’alisema Kipija,
Aliongeza
kuwa watendaji katika Halmashauri ya Kyela wamegeuka midomo ya mamba
kwa kutafuna fedha za umma zinazotokana na michango mbalimbali hivyo wao
kama madiwani hawatakuwa na huruma na watu kam hao,
Afisa mtendaji wa kijiji
hicho cha Ipinda Bonifasm Kayuni anayetuhumiwa kwa kosa hilo,mbari na kukiri kuwepo na kosa hilo aliomba msamaha na kudai
kuwa waliomsababishia kosa hilo ni
wasaidizi wake na kwamba kwa kuwa
yeye ni afisa mtendaji wa kijiji husika na kosa limeonekana kwake hivyo aliomba
msamaha ambapo msamaha huo uligonga mwamba,
Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Kyela Abdarah Mfaume kwa upade wake alisema kuwa ndiyo
Afisa mtendaji huyo amekutwa na hatia na kwamba sheria za
Kazi zinasema mtumishi
akikutwa na hatia inatakiwa ashushwe cheo au afukuzwe kazi na wao walifuata
sheria hiyo ya kumfukuza kazi kwa kuwa cheo alicho kuwa nacho ni cha chini,
Aliongeza kuwa kutokana na
afisa huyo kuwa na cheo cha chini waliazimia kumfukuza kazi kitendo kilicho
pingwa na madiwani ambao wametoa pendekezo la kumfikisha mahakamani ili hatua
zaidi za kisheria zifuatwe ili iwe fundisho kwa watendaji wengine wabadhirifu
na yeye amefuata agizo hilo ambapo tayali mtuhumiwa amefikishwa
katika vyombo hivyo vya kisheria,
‘’Baada ya tume kuleta majibu na yeye kukili kosa
sisi kama waajiri tuliazimia kumfukuza kazi
kutokana na kanuni ya sheria za kazi,lakini madiwani wametaka afikishwe
mahakamani kwa hatua zaidi ambapo sisi tumefuata agizo la madiwani kwa kuwa
ndio wenye Halmashauri,’’alisema Mfaume,
Mfaume alisema kuwa pamoja na kuazimia kumfukuza kazi afisa mtendaji huyo kwa kosa alilolitenda tayari amefikishwa katika vyombo vya sheria kama
walivyotaka madiwani.
Na Ibrahim Yassin,Kyela
No comments:
Post a Comment