Mshambuliaji wa Uruguay na Napoli, Edinson Cavanni
Katika taarifa ya jana usiku, Radio Marte ilitangaza: “Tumepokea taarifa kutoka ofisini kwa vyanzo vya kuaminika kwamba, Napoli imekubaliana dili la kuiuzia Chelsea Cavani.
“Rafa Benitez pia amebariki, lakini kabla ya kutangaza rasmi, Napoli inataka kupata mshambuliaji atakayeziba pengo la Il Matador.
“Aurelio De Laurentiis”, klabu itasomba kiasi cha Euro Milioni 58, sawa na dili la Ezequiel Lavezzi kwenda PSG mwaka jana.
“Mchezaji huyo atajiingizia mshahara wa Euro Milioni 8.5 kwa msimu pamoja na haki za picha,”. Habari zimevuja kama kwamba Cavani ametangaza anataka kukutana uso kwa uso na Rais, Aurelio de Laurentiis na kuna taarifa kwamba Manchester United nayo imo kwenye mbio hizo.
Mshambuliaji huyo wa Uruguayna baba yake awali walionyesha nia ya kutaka kwenda Real Madrid. Klabu hiyo ya Hispani iliwasiliana na Napoli, lakini sasa itabidi waipiku ofa iliyotolewa na Chelsea.
No comments:
Post a Comment