Tuesday, 25 June 2013

FELLAINI ATAKA PAUNI 100,000 KWA WIKI ARSENAL...KUMNG'OA EVERTON PAUNI MILIONI 22


KIUNGO Marouane Fellaini anataka kujiunga katika orodha ya wachezaji wanaolipwa Pauni 100,000 kwa wiki Arsenal, lakini The Gunners tayari imetenga dau kubwa kwa usajili mwingine.
Huku mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain akiwa njiani kutua kwa dau la Pauni Milioni 22, The Gunners wataelekeza nguvu zao katika kuboresha safu ya kiungo.
Raring to go: Marouane Fellaini is keen on joining Arsenal
Tayari kuondoka: Marouane Fellaini anataka kujiunga na  Arsenal

Fellaini ametokea kuwa mshindani mkuu wa nafasi mbele ya zoezi la Arsene Wenger kusaka kiungo, lakini dau kubwa linalotakiwa linaleta kama uhamisho huo utafanikiwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye kwa sasa analipwa Pauni 75,000 kwa wiki Everton, anataka kukuza kiwango chake cha sasa mshahara.
Kutoka kikosi cha sasa cha Arsenal, ni Theo Walcott na Lukas Podolski peke yao wapo katika kiwango cha mshahara cha Pauni 100,000 kwa wiki.
Mbali na kudai mshahara mkubwa, Arsenal pia watalazimika kufika bei anayouzwa Fellaini, Pauni Milioni 22- ambayo itafanya dili zima la usajili wake liendee kwenye Pauni Milioni 50.
Powerhouse: Fellaini could bolster Arsenal midfield
Injini: Fellaini anaweza kuboresha safu ya kiungo ya Arsenal
Target: New Everton boss Roberto Martinez faces fight to keep Fellaini
Mtu muhimu: Kocha mpya wa Everton, Roberto Martinez anakabiliwa na changamoto ya kumbakiza Fellaini

Na wakati Wakuu wa Arsenal wanataka huduma ya Fellaini majira haya ya joto, inafahamika kwamba watalazimika kufika bei inayotakiwa.
Zaidi ya hapo, Fellaini anataka uhakika wa kucheza katika safu kuu ya kiungo Uwanja wa Emirates. David Moyes alikuwa anamtumia kama mshambuliaji wa pili Everton.
Zenit St Petersburg, ambayo ina fedha za kumwaga, kiasi cha kuweza kufika bei ya Mbelgiji huyo, itatoa upinzani kwa The Gunners katika kuwania saini ya Fellaini.
Manchester City pia imeonyesha nia ya kumsajili Fellaini, lakini ilipunguza kasi tangu Yaya Toure asaini kuongeza Mkataba.

No comments: