Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema ataendelea kuisaidia klabu hiyo kama kawaida.
Kaburu amesema ataendelea kufanya hivyo kama mwanachama wa Simba na ana haki ya kufanya hivyo.
“Kweli mimi si kiongozi wa Simba, lakini ni mwanachama wa Simba na nina haki ya kuendelea kusaidia klabu yangu.
“Sidhani kama ni sahihi kujiuzulu halafu nisuse na kukaa pembeni hata katika sehemu ninayoamini ninaweza kufanya kitu ambacho kitaisaidia Simba.
“Watu wamesahau kuwa kabla sijawa kiongozi nilikuwa nikifanya hivi kwa ajili ya mapenzi yangu makubwa na Simba.
“Sasa nimetoka kwenye uongozi, basi ndiyo nikae pembeni kabisa. Kwangu naona si sahihi na nitaendelea kusaidia kila nitakapoona kuna nafasi au nalazimika kufanya hivyo kwa maslahi ya klabu yangu,” alisema Kaburu.
Kaburu alibwaga manyanga nafasi hiyo ya makamu mwenyekiti miezi michache iliyopita.
Hivi karibuni amekuwa akionekana katika mazoezi ya Simba na kiasi fulani baadhi ya mashabiki na wanachama wa Simba wamekuwa wakihoji kutokana na uwepo wake huo.
No comments:
Post a Comment