Na Ibrahim Yassin, Kyela
TAMASHA la uzinduzi wa mradi wa kupinga ukatili wa
kijinsia uliofanyika katika uwanja wa John Mwakangale Wilayani Kyela Mkoani
Mbeya umechukua sura mpya baada ya kufanyika kwa mchezo ya ngoma za asili na
mpira wa miguu huku wakazi wa kyela wakipokea kwa mikono miwila uzinduzi huo.
Uzinduzi huo ulifanyika jana kwa udhamini wa Shilika
lisilo la Kiseikali linalojishughurisha na kupinga ukatii wa kijinsia kwa
wanawake kwa kushiriana na Shilika linalolea watoto yatima na wale waishio
katika mazingira magumu wilayani hapa The Mango Tree ulilenga kufungua ofisi
kwa lengo la kuanza kutoa huduma hiyo katika wilaya ya Kyela.
Katika uzinduzi huo
kulifanyika mashindano ya ngoma za asili aina ya ling”oma kati ya Ndandalo na The amazon chaka zote za mjini ambapo
ngoma zote zilitoka suruhu na kutunukiwa Kitita cha Tsh,100,000.Kwa kila ngoma.na
pia kulifanyika mchezo wa kuigiza uliofanywa na kikundi cha Kasenyenda Group
chini ya Comred Katering ambao walizawadiwa Tsh,100,000.kutokana na kuigiza
vizuri.
Baada ya hapo ilipofika saa
10.30 jioni kulifanyika mpambano mkali wa kukata na shoka kwa kuzikutanisha
timu pinzani kati ya stend fc na timu ya Mazombi fc,(Mavampire)katika mpambano
huo lefarii wa kati alikuwa ni Ambwene Mwaipatania akisidiwa na Lain one Alliud
Mwang”onda na lain two Joseph Fongo (Collina).
Mpira ulianza kwa kasi huku
kila timu ikilisakama lango la mwenzie lakini ilikua ni timu ya Stendi fc
iliyofanikiwa kupata bao la kwanza na lamwisho kwa njia ya penalt lililofungwa
na Willy Mwasika Viera dakika ya 30 kipindi cha kwanza baada ya mchezaji hatari
Six Mwasekaga kuchezewa rafu eneo la hatari bao lililodumu hadi daika 45 za
kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa
kasi huku kila timu ikifanya mabadiliko ili kujiboresha zaidi kwa upande wa
timu ya Stendi fc waliwatoa Fred
Mido,Willy Mwasika na kuwaingiza Ally Martin na Salum Azizi, na Timu ya Mazombi
fc waliwatoa Anton Maiko na Fuguto Juma na kuwaingiza Baraka Kajo na Shapy
Mwakalonge.mabadiliko hayo yaliongeza mashamsham uwanjani hapo huku mashabiki
wa kila upande wakupuliza mavuvuzera kutokana na mchezo mzuri.
Wachezaji wawili wa timu ya
Mazombi Mpoki Mwakinyuke na Dulla Mwantuke walipewa kadi za njano kufuatia mchezo
mchafu uwanjani hapo,huku hadi dakika 90 za mchezo timu ya Stend fc ilitoka
kifua mbele kwa kuongoza goli 1.kwa 0,dhdi ya Mazombi Fc.
Timu ya Stendi fc walipata
zawadi ya kikombe,jezi seti 1,mpira na fedha taslim Tsh,100.000.na Timu ya
Mazombi walipata Kikombe kidogo,seti 1ya jezi,mpira na Fedha Tsh,50.000.zawadi
zilizokabidhiwa na mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreti Malenga ambaye alikuwa ni
mgeni rasmi huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Gabriel Kipija na
wenyeviti wa Serikali za mitaa na wakuu wa Idara katika Halmashaur ya Kyela.
Akizungumza mara baada ya
Tamasha hiloMkurugenzi wa Shilika la The Mango Tree Andilile Mwambaraswa alisema kuwa
lengo la kukutana ni kutamburisha mradi huo kwa jamii kwa ajili ya kupinga
ukatili wa kijinsia ambao utafanyika kwa kushirikiana kwa pamoja kati ya
Serikali,Asas ya The Mango tree kwa ufadhili wa Henry Jakson Foundation Medical
Research Internation kupitia Water Reed na Wilaya ya Kyela imechaguliwa kuwa
moja ya mfano katika utekelezaji wa mradi huu wa kupinga ukatili wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment