Na Ibrahim Yassin,Kyela
MSICHANA
Enita Kalota (23 Mkazi wa kijiji cha Mwalisi kata ya Ngana wilayani Kyela
amekutwa amekufa katika maeneo ya kijiji cha Ngana kitongoji cha Kandete kata
ya Ngana huku akiwa amenyofolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili,
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi eneo la tukio kaimu ofisa mtendaji wa kata hiyo ya
Ngana Joseph Mapunda alidai kuwa ofisi yake ilipata taarifa za kuwapo mtu
aliyeuawa katika kijiji hicho cha Ngana mnamo majira ya saa 3 asubuhi jana na
baada ya hapo walitoa taarifa kituo kidogo cha Polisi cha Kasumulu,
Alisema msichana
huyo alikuwa anaishi Boda ya Kasumulu baada ya kumaliza shule darasa la saba
mwaka jana katika shule ya msingi ya Mwalisi na kuwa jana walishangazwa baada
ya kuuona mwili wa msichana huyo akiwa amefia katika kijiji cha Ngana,
Mapunda
alifafanua kuwa walivyoutizama mwili wa msichana huyo walikuta baadhi ya viungo
vyake vikiwa havipo kama sikio na ngozi ya kisogoni vikiwa imeondolewa huku
kukikwa na tetesi kuwa hata sehemu zake za siri nazo zimeondolewa
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Ngana Stanley
Shimwela alisema kuwa tukio hilo limewashitua sana wananchi wa kijiji hicho
ukichukulia hilo ni tukio la tatu kwa mwaka huu wa 2013 ambapo vifo vyote
uhusishwa na imani za kishirikina baada ya maiti zote zilizouawa kunyofolewa
baadhi ya viungo vya mwili,
Mganga wa
zamu katika hospitali ya wilaya Kyela aliyeufanyia uchunguzi mwili huo
Dkt,Nsubiri Mwansule alisema kuwa baada ya wao kuufanyia uchunguzi mwili huo
walibaini msichana huyo kupigwa na kitu chenye ncha kali eneo la kichwani
kilichopelekea maumivu makali na kupelekea kifo,
Alisema kuwa
hawezi kusema lolote juu ya kutokuwepo kwa baadhi ya viungo ambavyo havipo katika
mwili wa marehemu kwa madai kuwa yeye si mmsemaji wa hospitali hiyo,
Kaimu mganga
mkuu wa hospitali ya wilaya Dkt Apaisaria Rumisha alipotafutwa ili kulitolea
ufafanuzi jambo hilo hakuweza kupatikana kwa madai kuwa yupo katika ofisi za
halmashauri ya wilaya kwenye kikao.
No comments:
Post a Comment