Friday 2 August 2013

MAANDALIZI ya kambi la vijana walio chini ya umri wa miaka 18 yamekwisha kamilika wilayani Ileje mkoani Mbeya

MAANDALIZI ya kambi la vijana walio chini ya umri wa miaka 18 yamekwisha kamilika wilayani Ileje mkoani Mbeya ambapo yatafanyikia Isoko kata ya Kafule kwa ya muda wa siku nne. Akizungumza na MBEYA LEO mkurugenzi wa kambi hilo Raia Mbembela alisema kuwa ghalama zake ni kiasi cha shilingi 570,000 katika kulikamilisha ikiwa ni kununua vifaa vya michezo kama Mpira Jezi na vinginevyo. Mbembela alisema kuwa jina la timu ni Chui Akapango ambapo litakuwa likisadifu kuacha historia katika vijana hao na kwakuwa wapo tiali katika kushiliki kucheza mpira ili kuweza kuinua vipaji vyao. Aliongeza kuwa dhumuni kubwa la kuinua vipaji hivyo vya watoto ni kuwa weza kufika hadi katika vilabu vikubwa kama vile Plizoni B, Mbeya city kwa kuwa wapo tiali kucheza kwa kujituma. Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Rosemary Senyamule alisema kuanzishwa kwa kambi hilo kutawasaidia wananchi wa wilaya hiyo kuwa na kipaumbela katika michezo na hususa ni kwa vijana hao walio chini ya umri wa miaka 18. Senyamule aliongeza kuwa michezo ni ajila kwa vijana na ni afya pia katika maisha ya binadamu ambapo vijana wanaweza kuondokana na tama mbaya kama vile kunywa pombe, tamaa mbaya za mapenzi na vitendo vya ukatili. Katika kambi hilo mkuu wa wilaya hiyo aliwachangia vijana hao kiasi cha shilingi 150,000 ambazo zilitumika katika kununua jezi za kuchezea mpira. Naye kapiteni wa vijana hao Olea Kibona alisema kuwa vijana hao wapo tiali katika kujitoa kimchezo na kuwa wanahamo ya kuweza kwenda kuchezea vilabu vikubwa. Alisema kuwa vijana hao wapo tiali kucheza kwa namna yoyote ile ilimuladi waweze kufika malengo yao waliyo kuwa wakitalajia na kuwa wanandoto kuwa wachezaji wakubwa ambao watakuwa na moyo wa kulitumikia taifa lao. Mdau mwingine wa mchezo wa mpira wa miguu Injinia Laison Mkondya alisema kuwa wapo tiali katika kufufua vipaji vya vijana hao na kuwa wanaweza kucheza kwa kujituma. Alisema kuwa vijana hao wanauwezo wa kucheza na kuweza kutoa hamasa kwa vilabu vikubwa kwenda kutembelea vijijini kuliko wanapo chukua vijana wa mjinin huku wa vijijini wakiwa wamesaulika. Na Eliud Ngondo, Ileje

No comments: